Tukubalieni, hii ni awamu ya sifa na kuvunja sheria

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Nianze kwa kusema kwamba watanzania tuna bahati mbaya sana. Maelezo yangu walau yatalinganisha awamu ya nne ya utawala wa nchi yetu na hii ya tano. Kwanza tukubali kuwa binadamu siyo mkamilifu hii ni tabia ya asili kwa binadamu wote wakiwemo hao tuliowapa mamlaka ya kutuongoza wa awamu hii ya tano. Hata hivyo hali hio haindowi wajibu wa kukosoa.

Kuna madhaifu mengi yalisemwa kuhusu awamu ya nne ikiwemo ulege lege wa maamuzi na watu kulindwa. Lakini yote hayo yalifanyika chini ya misingi ya kulindwa KATIBA. Ilikuwa ni udhaifu tu wa kibinadamu kulikochagizwa na kulindana na mazoweya ya uluwa wa madaraka. Kuna mambo mengi hayakufanyiwa kazi ingawa yalijuikana kwa mfano orodha ya wanaojihusisha na madawa ilikuwepo kwa awamu zote zilizopita lakini hatukuona hatua za maana. Ilifika wakati mkuu wa nchi akasema orodha anayo.

Haikutosha hata sakata la wazi la wizi wa fedha za Escrow na baadhi ya ufisadi ulifichwa na kukingiwa kifua. Ilisikitisha kuambiwa waliochota fedha warejeshe tu. Sijui umakini wake lakini walau zilirejeshwa na watu waliheshimiwa utu wao. Sio kwamba napongeza hapana, hapa nasifu ule msemo wa bora nusu shari kuliko shari kamili. Kwa ufupi awamu ya nne ilikuwa na lukuki ya madhaifu lakini katika kufuatwa misingi mikuu ya kikatiba walau waliheshimu haki za wengine.


Awamu ya tano sote tunajuwa kuwa uongozi wake (rais) ulikuja kwa bahati (by Chance ) ingawa wenyewe hawataki kuambiwa hivyo ukweli utabaki hivyo. Nasema watanzania tuna bahati mbaya kwa sababu watawala walituaminisha kuwa dawa ya matatizo yetu imepatikana ikawa ni kujazana sifa na kupongeza tu. Wasomi na wataalamu wetu wakanyamaza kimya. Viongozi wa dini wanasifia na kuwalinda watawala wetu kwa kila wafanyalo.

Sitaki kuamini kuwa kuna uweledi kwa kutumbuwa watu kabla ya kuthibitisha makosa yao na hili awamu hii umelifanya. Ilifika wakati hata kujali staha za watu na haki zao za msingi za kuheshimiwa zilipuuzwa. Wakati ule tuliita uanagezi. Kumbe sivyo. Picha inajidhihirisha kuwa ama kulikuwa na sifa katika utumbuaji, visasi, ubabe na kuvunjwa sheria. Hali imeendelea ya kuchaguwa mambo ya kufanyia kazi tena kwa staili ile ile ya sifa, ubabe, visasi na kuvunjwa sheria. Tumeshuhudia maagizo yaliyowapita vimo hao wanayoyatowa .Yaani kunguni anabeba lumbesa? Ubaya yanafanywa haya sheria na katiba hazizingatiwi. Haya ya sasa ya Mkuu wa Mkoa kujibebesha uwezo wa kipolisi wa kushughulikia madawa ya kulevya yanachefuwa. Tunastuka watu wanavunjiwa heshima bure bure kumbe utaratibu wa kufuatilia uliowekwa na sheria upo lakini haukufuatwa. Baya zaidi mamlaka za kufuatilia zilizowekwa kisheria zipo lakini kumbe hata uongozi wa nchi haujuwi na ndio hawa walioapa kuilinda KATIBA. Haya yanafanywa wakati washauri wa kisheria wa serikali wapo, waziri mwenye dhamana ya sheria yupo na wasaidizi wengine wapo. Hatimae baada ya madhara anateuliwa kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya. Sasa watu wanashtuka lakini madhara tayari yamepatikana.

Yako mengi ya kuvunja sheria yanalalamikiwa ikiwemo zuio la mikutano ya kisiasa na kuingiliwa mihimili mengine ya dola na serikali. Hili sijui undani wake lakini linasemwa lipo. Kwa nini yote haya yanatokea na kujirudia? tukisema hii ni awamu ya sifa na kuvunja sheria tunakosea kweli ?

Baadhi ya wataalamu walishaonya kuwa hatua zichukuliwe mapema kabla athari hazijaenea. Wanasiasa wao walionya mapema ikiwa watu wanafikiri kuwa yatawahusu wapinzani tu sawa. Leo tunaona hata Bunge linashtuka japo kinafiki. Sikwambii wafanyabiashara na wakwezi wote.

Kuna haja ya kujitafakari tena. Awamu hii ni dhahiri ni ya sifa na kuvunja sheria.

Kishada.
 
Back
Top Bottom