barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Sipo huko "instagram" lakini nimekuwa nikipata "update" za huko kupitia hapa au hata kuona baadhi ya "screenshot" zenye maandishi na picha ya kinachoendelea huko. Nasikia huko umaarufu unatokana na mtu kuwa na idadi kubwa ya wanaokufuatilia.Idadi hiyo inaongezeka kutokana na habari unazo-post.
Huyu mtoto (maana wengine tulikuwa washirika wa baba yake kikazi) amekuwa anatuma habari nyingi sana za ndani ya kapeti. Kwa kweli nyingine ukiziona zina ukweli wake japo nyingine hazina ukweli.
Lakini kwa sababu tayari ana wafuasi wengi na kwa vile anayewaongelea wamekuwa kwa sasa hawapendwi au wamepoteza umaarufu, basi chochote ukisema mwingine kinyume na huyo binti,basi tegemea matusi sana toka kwa "wafuasi watiifu" wa huyo binti.
Bahati mbaya au nzuri na yeye amewajenga "wafuasi" wake katika muktadha wa kujibu hoja jumlisha tusi.Yaani anaweza kuwa na hoja nzuri tu,lakini lazima isindikizwe na matusi ya maana tu.
Anaweza kuwa na hoja nzuri tu kuhusu Bashite, lakini lazima hoja hiyo iambatane na matusi ya nguoni, anaweza kuwa na hoja nzuri tu kuhusu aina ya uongozi wa JPM,lakini hoja hiyo lazima iambatane na tusi. Hii si sawasawa...Hii si sawa
Na kwa sasa amekuwa kama "Authority".Sikatai,lakini pia watu wawe makini na aina nyingine ya habari. Sio zote anazokuwa anatoa zinaweza kuwa za kweli. Na wale walioumia sana wakati ule akimtukana braza Eddo, maumivu ya matusi yale ndio wanayapata hawa wanaotukanwa kwa sasa.
Tukiwa jamii inayotengeneza watu wa ustaarabu wa mijadala,tukubaliane na habari anazotulisha, ila tutafotiane na aina ya "matusi" yanayoambatana na habari anazozirusha.
Kwa mfano ile ya gari la kwenye kontena bandarini,ukiangalia gari ya kwenye kontena haina namba,lakini gari anayoisambaza yeye kuwa ndiyo ilikuwa kwenye kontena ina namba zenye usajili wa Zanzibar.Mimi mpaka sasa sijajua hoja kuu hasa ni nini?
Inawezekana kweli ile ilikuwa "kick" ya JPM kupoteza habari ya Napelembe Moses Nnauye,lakini kuna haja ya kupotosha kwa kuweka gari isiyokuwepo ktk kontena?Yaani ye huyu binti kwanini aweke gari ambayo siyo yenyewe?
Lakini kwa sasa inabidi usihoji, unaweza kumuuliza hata mkeo akakwambia "Mange kasema",ukimuuliza kwani akisema huyo ndio ukweli usio na shaka?Atakwambia yule anajua kila kitu,hata wewe akipewa jina lako anakuchimbua mpaka kwa vimada wako...Asalaleeeee!!!Mwakubwa haya.
Toka kauli ya Rais kuhusu Kinana na India ilivyotoka.Tayari binti katengeneza story na kupata "wafuasi" lukuki.Kwamba Kamaradi Kinana kafungiwa,mara katumiwa usalama ili akae ndani bila kuongea na maneno kibaoooo.Hii kitu imeshasambaa na kuaminika kwa 95%.
Lakini ukweli ni kuwa Kinana yupo nje ya nchi,kama ni India au China hiyo si habari kubwa sana.Kwamba Mzee anasema "amemtuma kutibiwa India",siyo jambo la ajabu sana.Kama tumemvumilia Rais anaposema "ngombe" badala ya "Ng'ombe","ngangania" badala ya "ng'ang'ania" na "broken" nyingi tu katika Kiswahili,basi hata hili lisitusombe,muhimu ni kweli kuwa Kinana yupo India?
Kamaradi Kinana aliondoka kwenda ng'ambo,alikwea ndege ya Emirates,flight # EK726 aina ya B773 kupitia Dubai,siku aliyoondoka Kamaradi Kinana ndio siku aliyoondoka Mstaafu wa Bagamoyo,yeye aliondoka na Ethiopia,flight # ET804 aina ya B738 kupitia Bole Addis Ababa.Hawa wawili waliondoka siku moja kwa mashirika tofauti.
Kwamba kaenda kutibiwa,hilo si jambo la kulisemea,kwamba yupo nje ya nchi...hilo ni kweli.Sasa kwa sbb kashasema "binti" basi,na kwasababu wanaosemwa ndio wale waliopoteza mvuto,basi lolote wanalosemwa itakuwa ni kweli tena ukweli mtupu.
Tuko katika ulimwengu wa "Post-Truth Politics",yaani ukweli huja baadae sana baada ya uwongo kutawala.Kipindi ambacho uongo hushika hatamu zaidi ya ukweli.Zama ambazo uongo wa kidijitali unasambaa kuliko ukweli wa kianalojia.Ni wakati wa kuchagua,kuchuja na kuamua.
[HASHTAG]#Mangekasema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#DadaWaNyaniNgabu[/HASHTAG]
Cc Nyani Ngabu