Tukubaliane kwamba hatuna vipaumbele vya muda mrefu kama taifa

Justice minister

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
1,173
823
Kukosa vipaumbele ni sawa na kwenda mahali usipopajua, wengine wanasema ni kukosa dira na malengo na matokeo yake unakua ni mtu wa kuendeshwa na nyakati, matukio na hali ya mazingira husika. Wachina wana usemi mmoja usemao kwamba "kama hujui unakokwenda, huwezi kupotea njia".

Hayo yanashabihiana sana na hali inavyokwenda nchini, hakuna anayefikiri Tanzania ya miaka 50, 100 au 200 ijayo. Wenzetu wazungu wanatengeneza katiba zitakazoendesha nchi zao kwa hata karne mbili lakini bongo hakuna anayefikiri Tanzania ya mwaka 2099 itakavyokuwa huku rasilimali za nchi zikiendelea kuvunwa na mabeberu, badala yake tumekuwa watu wa ku-deal na mambo madogo madogo huku mengi yakiwa ni matamko ya kisiasa yanayotolewa majukwaani na kufanywa ndio kama sera na dira ya serikali huku kila awamu ikija na slogan yake na kufanya mashindano kuonesha nani alikuwa zaidi.

Miaka zaidi ya 50 tangu uhuru wa bendera lakini hakuna hata jambo moja tunaloweza kusema tulilisimamia hadi likasimama. Kuanzia elimu, afya, kilimo, viwanda, utamaduni, biashara, mazingira, uraia kote tumeshindwa, awamu zote zimekuwa kama zipo kwa ajili ya majaribio na kwa kuwa hakuna anayejua anakokwenda tumekuwa watu kudakia mambo na kuyaachia njiani kwa kudhani kwamba ndio maendeleo. Mbunge wa vunjo mhe. Mbatia aliwahi kusema bungeni kwamba Tanzania haina mtaala wa elimu na kama angeoneshwa basi angejiuzuru ubunge. Hiyo maana yake ni kwamba hatuna elimu kwa sababu hatujaona umuhimu wake. Sote tunafahamu maendeleo ya mataifa ya magharibi yalijengwa kwenye msingi wa elimu, lakini sisi tunataka maendeleo bila kuwa na elimu(elimu kuhesabu degree)

Inawezekana tuna sera zenye nafuu lakini bado hatujawa na serikali iliyo siriazi inayoelewa nini inafanya na malengo yake. Nchi inaongozwa na matamko kama ndio sera za taifa, atakachosema rais ndio sera na sheria, hakuna stable management kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini kiasi cha kufanya kuwepo na miingiliano ya majukumu ambayo ni moja ya sababu zinazozorotesha utekelezwaji wa sera na mipango dira ya taifa.

Kwa mfano suala la serikali la kuhamishia ofisi Dodoma ni ahadi binafsi ya JPM aliyoitoa kwenye kampeni wala haikuwa ajenda ya kitaifa ukizingatia kwamba mpango huo uliasisiwa zamani wakati hakukuwa na teknolojia ya mawasiliano kama sasa inayoweza kuwakutanisha watu wakazungumza kama kikao huku kila mmoja akiwa ofisi kwake, na ndio maana Mkapa na baadae Kikwete hawakuona kama ni suala muhimu kama serikali ya sasa ya JPM inavyolichukulia suala hilo, na tatizo wala sio serikali ya JPM kuhamishia makazi Dodoma, tatizo ni kwa kuwa hakuna sera kwa sababu baada ya JPM kumaliza kipindi chake anaweza kutokea rais mwingine akasema serikali kuhamia Dodoma halikuwa jambo muhimu na lenye tija hivyo ataamua kurudisha ofisi Dar es salaam kwa sababu mamlaka yake ndio sera na sheria ya nchi hivyo kupoteza muda na rasilimali nyingi kushughulikia suala hilo.

Vipaumbele ndio dira ya Taifa na kila mwananchi anatakiwa ajue nini anafanya kwa ajili ya nchi yake, makelele ya kisiasa hayajengi nchi. Ni matumaini yetu kwamba serikali itabuni na kusimamia dira ya taifa kwa kutathmini maendeleo ya taifa ya muda mfupi na mrefu na kuhakikisha tunakuwa na katiba inayoendana na changamoto za utandawazi huku kila awamu itakayoshika madaraka itahakikisha vipaumbele hivyo vinatekelezwa na kuachana na maneno ya majukwaani yanayochukuliwa kama ndio dira na sera ya nchi.

Uzalendo kwanza.
 
Hii nchi hata kungekuwa na katiba nzuri kiasi gani kwa hawa wanasiasa wetu lazima wataiweka pembeni na wataongoza kulingana na vile wanavyojisikia.
 
Hii nchi hata kungekuwa na katiba nzuri kiasi gani kwa hawa wanasiasa wetu lazima wataiweka pembeni na wataongoza kulingana na vile wanavyojisikia.
Hata katiba ya sasa pamoja ya kwamba ina mazuri lakini serikali imekuwa ikionesha kuidharau wazi wazi kabisa, kwahiyo hilo ni tatizo namba mbili likitanguliwa na katiba yenyewe.
 
Tatizo ni nchi kuongozwa na ilani ya chama cha kisiasa ambao unaputisha ba watu wasiokuwa na weledi ilimradi wana kadi ya chama au wajumbe wa chama cha mapinduzi, BADALA ya kuwa na mpango wa maendeleo wa taifa ambao kula kiongozi atakayekuwa madarakani either upinzani au chama cha sasa, sababu ni kuwa mpango wa maendeleo wa sasa ni wa chama kama ilani
 
Vya muda mrefu umeenda mbali sana, kama bunge linaweka bajeti ya mwaka halafu mtu mmoja anaikanyaga na kuivunjavunja, utasemaje hatuna vipaumbele vya muda mrefu?

Hata vya muda mfupi hatuviwezi!
Mkuu hata hiyo bajeti ya mwaka serikali haiwezi kuikamilisha bila misaada wakati rasilimali zipo. Tatizo kila rais anakuja na lake kichwani, wanafanya mashindano bila mipango. Si unaona hata suala la kuhamia Dodoma halipo kwenye vipaumbele vya taifa. Hakuna maendeleo, kweli pombe haileti maendeleo.
 
Back
Top Bottom