OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,084
- 114,611
Majuto ni mjukuu,asiyesikia la Mkuu huvunjika guu!Katika mambo ambayo wapiga kura wengi hawazingatii sana ni majuto ya miaka mitano ikiwa watachagua rais na chama kibovu.Nchi imepigwa ganzi kwa sasa hatuna pa kushika,within a minute tumepoteza uelekeo.Muheshimu Mbowe na wafia nchi wengine walisisitiza sana nchi iwe na dira mahsusi itakoyosimamiwa na kila kiongozi atakayeingia madarakani bila kujali chama.Tumeacha ombwe ambalo mtu anaweza kuingia madarakani na akaleta ya kwake,nchi inaweza kupata kiongozi mfano wa Mfalme Juha na akadidimiza kila mtu!Sasa katika kipindi kifupi tumeinjoi sana mikogo na maigizo bila kuonyeshwa ni wapi hasa tunaelekea.Maigizo hudumu kipindi kifupi sana.Sote tunaona yanayoendelea na impact yake kwa kesho.Kwa kuwa aina ya watu tulionao sio wasikivu kabisa,tukubaliane kwamba tupo kwenye kipindi cha mpito...tuendelee kuinjoi maigizo mpaka 2020