Tukubali tukatae Tanzania ni taifa la shamba la bibi

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,215
56,855
Hii ndio hali halisi, Rushwa itangazwe kuwa ni janga kubwa linalotakiwa kutazamwa kwa jicho pevu. Kwa upigaji Tanzania hatuwezi kushika mkia ni namba za mwanzoni, binafsi nimeanza kuona kila Mtanzania ni mpiga dili tu nikiwemo na mimi! Ukikaa vibaya halafu hela nje nje inakula kwako. Si Escrow au EPA Tanzania lina watu wapigaji hata tusipoangalia kabila n.k

Hili tatizo bado halijapata muarobaini hasa ngazi za juu! Naona Mambo ndo yanazidi kuharibika. Ni dhahiri kunahitajika intelligence juu ya haya mambo lasivyo tutakufa maji. Hakuna cha kusema ni CCM wala nini hili ni tatizo! Na linatakiwa kudhibitiwa hata chama chochote kitakachoingia madarakani kikute tatizo limetibiwa sio nao waje warithi twafa.
 
True upigaji atujambo wasi wasi Wangu uko juu ya hii miradi mizuri iliyoanzishwa kwa nia nzuri ikaishia mifukoni mwa watu,maana tumeyaona kwa nyerere alianzisha vingi vililiwa na mchwa.Walioona sekta binafsi ndo iachiwe shughuli za uchumi waliyajua haya maana mtu ni mkali Sana kwenye chake kuliko cha umma
 
Lazima kwa sasa tuseme ni MBOGAMBOGA kwakuwa wao ndiyo wanaliongoza hili Taifa tokea UHURU,wengine hawajawahi,kuwahukumu ambao hawajashika dola ni kusema nchi haina aliyebaki akiwa ni muadilifu wakati si sawa.
Sikubali kuwa samaki wote wakioza basi ni sote,kama ni hivyo,TUWEKE SULTAN.
 
Mtoto ambaye kila siku yuko na baba halafu anakuja kufanya jambo bila kumwuliza baba ni wazi kuwa babake huwa hufanya hivyo bila kumshirikisha mtu mwingin anayepaswa kushirikishwa
 
Upigaji sio wa kabila fulani wapo wengi ambao wamejificha. Sio sahihi kutumia tribal sentiments kuwaonea wananchi wa kabila fulani waonekane kama kielelezo cha ufisadi Tanzania.
 
Back
Top Bottom