Tukiwa tunafanya mambo mbalimbali tunatakiwa kujiuliza maswali haya..

mxsdk

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,585
2,049
TUKIWA TUNAFANYA MAMBO MBALIMBALI IWE MBELE ZA WATU AU TUNAPOKUWA PEKE YETU NI VIZURI KUJIULIZA HAYA MASWALI:

1.Kwanini nafanya hiki kitu?
Hapa hakikisha unapata jibu la kwanini ufanye.
2.Nataka nifanikishe kitu gani katika kufanya hiki kitu? Yaani unapofanya kitu unataka matokeo yawe nini?
3.Ili iweje?
Hapa ni lazima tujue tunafanya na kuna matokeo ya kufanya hicho kitu sasa unataka hayo matokeo ili iweje.
4.Unapata nini?
Nikishapata matokeo ya kile ninachokifanya yananifaidishaje mimi.
5.Najifikiriaje?

Hapa ni lazima ujue kwanini wewe ufanye hicho kitu? Wewe ni nani hadi ufanye hicho kitu nk. Baada ya kujiuliza haya maswali matano tutagundua kwamba kitu ambacho tunataka kufanya ni cha kijinga au kina maana na umuhimu. Kabla hatujafanya chochote ni vyema sana kufanya tathmini ili isitokee tukafanya kitu na kuonekana aidha wajinga, washamba au uwezo wa kufikiri mdogo. Kuna vitu vingine vinafanyikaga vya kijinga sana lakini sababu ni kwamba aliyefanya alifanya tu hakutafakari kujua kama kuna umuhimu wa kufanya au hamna.

Mfano unakuta mtu anajisifu kuwa na kitu fulan kinaweza kuwa material thing au uwezo fulani aliopewa na Mungu kiakili au kimawazo, basi anajikuta tu anajiinuainua, mazungumzo yake ni kujiweka katikati ya mbingu na nchi yani kwa kifupi anakuwa ni tatizo sio baraka tena na anajisahau kabisa. Kwanini? Shida ni kutokuchuja kwamba nifanye hiki kweli? Kama nifanye basi nifanye ili iweje Hana action plan,anafanyafanya tu. THIS IS NOT RIGHT.

Kama Mungu ametupatia kitu nafikiri tungevitumia hivyo vitu kwaajili ya utukufu wake. Kwa mfano Wengine tumepewa simu tu lakini vile imekuwa tatizo ni bora tusingekuwa nayo,hiyo simu hata mama yake hagusi na akigusa atapewa maelekezo hayo ambayo hayana unyenyekevu ndani yake. Napata kuwaza hii ni simu mtu hatulii je akipewa ule muujiza anaoombaga itakuwa ni kivumbi sio. Vitu vingine hata sio vya kuombea ni kujiendekeza na kaushamba kidogo.

LETS DO IT RIGHT FRIENDS.
 
Back
Top Bottom