Tukiwa outing anageuka bubu

Joined
May 3, 2015
Posts
8
Reaction score
5
Wakuu,

Ninakwazwa na tabia ya binti mmoja hivi ambae nimempa heshima kubwa ya kumtoa outing sehemu ya daraja la juu ambapo hata mimi huwa siendi. Huyu binti yupo kwenye middle-class anaishi na wazazi wake na ni mhitimu wa chuo.
Mimi ni mjasiriamali nina duka la jumla huku uswahilini na pia najihusisha na kilimo cha mchele mkoani, nilipomaliza nilisota sana benchi nikaamua kuwa mfanyabiashara na sasa mambo yapo levo namalizia nyumba Bunju.

So nikasema acha nitafute mtoto mzuri msomi niwekendani nikampata mtoto mmoja hivi mkali sana akakubali kimsingi kuwa na Mimi hatujazini bado. Lakini kuna jambo bado sijalielewa kwamba tukiwa outing haongei chochote mm ndo nageuka muongeaji mkuuNikikaa kimya basi ndo tunakua kama mabubu vile.

Tena unakuta nimejikoki nimempeleka sehemu ya maana na tulivu lakini ni yale yale, nikianzisha habari za Mkurunzinza kufurumushwa Burundi ambazo ndio zilikua zina trend hii wiki nzima iliyokwisha anakuuliza Mkurunzinza ndio nani.Nikisema nianzishe story za Escrow na bunge ambazo msomi yoyote hapa Tz hawezi kushindwa kujua.

Unakuta yupo kimya nikisema haya sasa ngoja nizungumzie mapenzi ambayo ndio yametuleta hapo date pia kimya nikimuuliza kama ananipenda anasema ndio. Haya myweather na manny wamepigana majuzi ulilionaje pambano? Ananiuliza ni akina nani hao.

Hivi wadau mkiwa date ni lazima watu muongelee mapenzi mwanzo mwisho?Au kwenye date kama hii ambapo mpenzi anakaa kimya mwanzo mwisho unafanyaje? Au hanipendi?


 
Tatizo huna maneno mazuri ninaweza kumfanya bubu aongee
sasa wewe unaongea nae kama unaongea na mshkaji wake watoto wanapenda vitu vizuri bana
 
Yawezekana anakuogopa that's why hayupo comfortable kuongea
 
Kijana hizo topic unazozungumza naye kwa kweli si zenyewe kabisa, sijui hiyo outing mnaenda wapi lakini kuna mambo ya kuzungumza huko

1. Muulize maswali yanayomhusu yeye au mazungumzo yanayomhusu kama familia yake, anaonaje kuhusu maisha na mambo kama hayo. Sasa wewe mpo sehemu tulivu unauliza habari za boxing!!! kweliiiiii

2. Usiwe muongeaji sana mpe nafasi ya kuongea, isije kuwa unabaldili stori sana mpaka anabaki anakushangaaa tu.

3. Usiwe na mada/topics ngumu, sasa hiyo Escrow mpaka rais mwenyewe haelewi wewe leo unataka mtoto wa watu akueleze nini? Uliza vitu simple na mtaenda sawa tu. Muulize hata kuhusu nywele zake (kama anazo nzuri lakini) au hata pochi na mambo mengine. Kuwa msikilizaji zaidi na mfanye ali relax
 
msifie kwa maneno mazuri na mweleze hisia zako juu yake kwa mahaba. muulize hata mambo ya familia yake kwamba wapo wangap, future yake n.k
 
asipokujibu au akasema hajui ujue hana interest na wewe funga virago.
 
nijibu kwanza hili swali, je mnapokuwa pamoja huwa anachati au kubofya bofya simu yake?
 
Nliwahi kua Na bf nlikua namuogopa yaan nkiwa njian kwenda kuonana nae roho inadunda ka naenda kuona simba lol, Na nkifika bas me ni bubu akati naturally naongea kama kasuku. Hata sijajua kwanini hadi Leo.
 
Mkuu unaendaje Date na "Mtoto" unategemea nini?? Kuna mtoto anajua Escrow&Co ..?? umeshaona tatizo lilipo.!!!! haahaha Muulize mambo ya Tom&Jerry Ben10 dexta N.k uone kama hajui......!!!!
 
Pengine unamtoa sehemu zenye kiyoyozi kikali sana mtoe kwenye mazingira aliyoyazoea.

Unajua hapo atakua anaguna kwa ndani tu hawezi kuongea.
 
Nliwahi kua Na bf nlikua namuogopa yaan nkiwa njian kwenda kuonana nae roho inadunda ka naenda kuona simba lol, Na nkifika bas me ni bubu akati naturally naongea kama kasuku. Hata sijajua kwanini hadi Leo.

Vipi, ushamzoea? au ni mjeda!!!
 

Mkuu unajua zilikuwa zimebaki kama dakika tano kwenda lunch wakati nasoma hii comment yako, nimecheka sana imebidi niende tu lunch, eti escrow hata rais wa nchi haijui sasa unamuuliza kimwana kwenye date hahahahaha
 
fanya utaratibu wa kumtafuna kwanza wewe kijana mbona unakosa priority kwenye mahusiano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…