🧠 Tukio Si Tatizo, Tafsiri Ndiyo Tatizo

🧠 Tukio Si Tatizo, Tafsiri Ndiyo Tatizo

Joined
Apr 6, 2024
Posts
72
Reaction score
69
Chakula cha Ubongo na Psychology Leo #
Watu wengi hufikiri tukio ndilo linalotuumiza. Mwanasaikolojia Albert Ellis alionyesha kuwa si hivyo kupitia mfumo wa ABC:
A (Activating event): Tukio lililotokea
B (Belief): Tafsiri au imani yako kuhusu tukio
C (Consequence): Hisia na tabia zinazofuata
Mfano: Rafiki hajajibu ujumbe wako kwa masaa sita.
Tafsiri 1: "Ananipuuza." → huzuni, hasira.
Tafsiri 2: "Huenda ana shughuli nyingi." → utulivu.
Tukio ni lile lile, lakini hisia ni tofauti kabisa kwa sababu ya B.
Zoezi: Kesho ukihisi hisia kali, simama na ujiulize: "Nimeambiwa nini na tukio hili, na nimeongeza nini mimi mwenyewe?"
💡 Badilisha B, na C itabadilika.

Ukiwa na mawazo mazito au unahitaji mtu wa kuzungumza naye usibebe peke yako. Ushauri nasihi unaweza kubadilisha maisha yako.
RJ.COUNSELLING&PODCAST
📞 +255 788 241 191
🌐 R.J. Counselling & Podcast
📱 @robatjemsi
Hashtags: #ChakulaChaUbongo #AfyaYaAkili #UshauriNasihi #SautiYaNdani #Saikolojia #RobertJamesPodcast #Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom