Tukio La Kushangaza Eldoret: Mti Wa Mugumo Waanguka Kisha Baadaye Kidogo Ukanyanyuka

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
tree.jpg
https://www.standardmedia.co.ke/ure...he-fall-of-mugumo-tree-what-does-it-symbolize Wakenya wenzangu wanajua mti huu mtakatifu wa Mugumo, kwenye jamii ya Gikuyu, ukianguka huwa inamaanisha nini. Leo nimeona habari hizi za mti wa Mugumo ulioanguka Eldoret na wakazi wa sehemu hizo wakawa wanasimulia kwamba maishani mwao hawajaona maajabu kama yale yaliyotokea. Mti wa Mugumo ulianguka na hadi mizizi yake ikawa imetoka ardhini na baadaye kidogo ukanyanyuka nakurudi kama ulivokuwa hapo awali. Hili tukio limefanya niwaze kuhusu dini zetu za kale na sehemu yake kwenye maisha ya sasa. Hivi ingekuwa ni muujiza flani kwenye dini ya kikatoliki si sasa hivi wangekuwa wamewatuma makadinali kadhaa kutoka Vatican waje kudhibitisha tukio lenyewe? Je sisi kama waafrika huwa tunachukuliaje tamaduni zetu? Kama za maana au kama upuuzi wetu wa jadi tu? Maoni yenu wakuu.
 
huo mti ukianguka huwa unaashiria nini mkuu?Au mizimu ya Dedan Kimath haifurahishwi na mafisadi wanavyotafuna keki ya taifa wkati wao walipoteza maisha sababu ya uhuru
Wazee huwa wanasema ukianguka huwa unaashiria kwamba tukio kubwa(positive au negative) linabisha mlangoni. Mti wa Mugumo ambao ulikuwa una miaka 300 ulianguka ghafla kabla ya Kenya kupata Uhuru.
 
aisee tunawaombea liwe tukio jema
Haujaanguka kabisa mkuu, ukianguka watu huwa wanapanick sio mchezo. Kondoo huwa wanachinjwa na pombe za kiasili huwa zinapikwa. Kuna tetesi kwamba wanaume wote kwenye sehemu la tukio huwa wanalazimika kuiona papuchi kwa umbali sanaaa, kwa wiki mbili hivi! Yaani waafrika sijui kwanini hizi dini zetu za jadi huwa tunaona aibu hata kuziongelea tu.
 
Wakenya ni wanga ila wako bize kunyooshea vidole nchi zingine.
 
Haujaanguka mkuu, ukianguka watu huwa wanapanick sio mchezo. Kondoo huwa wanachinjwa na pombe za kiasili huwa zinapikwa. Kuna tetesi kwamba wanaume wote kwenye sehemu la tukio huwa wanaiona papuchi kwa umbali sana, kwa wiki mbili hivi! Yaani waafrika sijui kwanini hizi dini zetu za jadi huwa tunaona aibu hata kuziongelea tu.
aahhah ahahha
 
Wakenya ni wanga ila wako bize kunyooshea vidole nchi zingine.
Mti wa Mugumo ulikuwa mtakatifu kwasababu babu zetu walikuwa wanafanya maombi kwa Mungu chini ya mti huo. Sio uchawi. Tena hawakuwa wanaabudu miungu, bali ni Mungu mmoja. Sanasana maombi yalikuwa yanafanyika chini ya mti huo wakati wa kiangazi. Huwa wanasimulia kwamba walikuwa wakikesha chini ya mti huo na wakati wa kuenda zao nyumbani mvua ulikuwa unanyesha.
 
Ninavyojua ni kuwa mugumo tree ni parasitic na hufyonza madini na chakula kutoka kwa host tree kwa miaka hadi miti yote ikaanguka, sababu ikiwa the host tree dies due to lack of nutrition.
 
Hii ni kwa wale ambao wameshiba kwa itikadi kali za kikristo na kiislamu, kiasi cha kupuuzilia kabisa uhalisia wa dini za jadi za kiafrika. https://en.m.wikipedia.org/wiki/Mugo_wa_Kibiru Someni mmfahamu nabii Mugo Wa Kibiru aliyetabiri ujio wa mzungu Kenya miaka mingi kabla ya mkoloni kufika pwani ya Afrika mashariki. Alitabiri pia kwamba mti wa Mugumo ambao ulikuwa Thika utakapoanguka mzungu atafurushwa Kenya. Mkoloni alipanick na kuogopa utabiri huo kiasi cha kuujengea mti huo 'support' ya chuma kote kote, ili usianguke lakini haikuzuia kitu. Mti huo wa Mugumo ulipigwa na radi ukanyauka hadi ukaanguka miezi kadhaa kabla ya Kenya kupata uhuru. Sio hadithi za vijiweni hizi, kumbukumbu hii ipo kwenye vitabu vya historia ya taifa la Kenya.
 
Back
Top Bottom