Tukiimarisha bandari zetu hatuhitaji misaada ya wahisani

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Bandari.jpg

SEKESEKE la ufisadi mkubwa wa kukwepa kodi uliofanywa na wafanyabiashara wakubwa na maofisa wa Mamlaka ya Bandari na Idara ya Forodha bado linaendelea na kesi iko mahakamani.

Lakini ni jana tu wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa mara nyingine alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano, hatua iliyomfanya ampe saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 jana jioni.

Ziara hiyo ya ghafla imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuzisimamisha kampuni 210 za wakala wa upakuaji mizigo bandarini kutokana na kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi mbalimbali zilizotokana na mizigo iliyopakuliwa.

Kufichuka kwa kashfa za ufisadi katika Bandari kumedhihirisha namna serikali inavyopoteza mabilioni ya shilingi kupita Bandari ya Dar es Salaam pekee kutokana na uzembe na ufisadi wa watendaji.

ZAIDI IKO HUMU...
 
Back
Top Bottom