Tukiendea hivi, ni miaka mingine 5 ya kupoteza

Pius J. Kiwarya Lema

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
1,097
566
Mimi natumia kichwa kufikiri, mtu akitimiza wajibu wake kwangu sio jambo jipya mfano mdogo tu unielewe kuhusu kodi kukusanya kodi ni wajibu sio ombi kama walikuwa hawakusanyi kodi ni uzembe/wizi sio jambo jipya la kumpongeza wakati watu ni walewale mfumo ni ule ule.

Jambo jipya kwenye swala la kodi la kupongeza ni kunionyesha vyanzo vipya vya mapato vya awamu ya tano ndo ntakuelewa, viko wapi? Labda tusubiri pili Rais Kikwete aliwasamehe baadhi ya wezi wa EPA wakarudisha fedha lakini hawakupelekwa mpaka leo.

Huyu amesamehe baadhi ya waliokwepa kodi Bandarini (makontena) akawapa siku saba walipe, wakalipa hatujasikia wamepelekwa mahakamani hawa Magufuli na Kikwete hawana tofauti yeyote katika eneo hili nipongeze nini? Namsubiri atekeleze wajibu wake kama anaweza kwa maoni yangu; Shekhe ni yule yule kanzu imebadilika.

Hivi nina furahia nini iwapo serkali ya CCM kupiitia shirika letu TANESCO walikuwa wanatuibia sh 6000/ na yeye akiwemo kwa ajili ya fomu ya maombi ya awali ya Umeme? Mwacheni Magufuli atimize wajibu wake, sio kumsifia mtu kwasababu hatakuibia tena.Ni miaka mingine mitano ya kupoteza kama tutaendelea kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe, ni vyema wakajua mabadiliko tuliyoyapigia kura ni ya kisera kisheria na kifkra .

Hadi sasa anachohangaika nacho Magufuli ni fikra kama wapizani (kuwaza) tu lakini hajafanikiwa kutenda kama wapinzani na nikilitizama hili Bunge la 11 ilivyopangwa sioni hayo mengine mawili yatapitia mlango upi? Maana kufanikiwa kwake kutategemea sana maamuzi yake katika kujenga (Strongly Institution) na siyo umaarufu wa mtu mmoja mmoja wa kutipua majipu badala ya kupambana na ufisadi tusidanganyane CCM ni Magufuli na Magufuli ni CCM.

Nawasilisha CCM ni ile ile
 
nothing new at all.hakuna cha majipu wala chunusi, anachokifanya ni kutoa waliowekwa na utawala wa zamani na kuwaweka anaowata yeye kama raisi mpya!!BTW it's a mindset issue because Anafanya tunayopenda kuyasikia na kuyaona ila siyo tunayotakiwa kuyasikia na kuyaona
 
Nilipoona "Lema" tu...nikajua hata sikusoma bandiko
Aina hii ya fikra ndio inayoifanya nchi hii isote badala ya kukimbia ktk kutafuta maendeleo! Kuna uhusiano gani kwa hoja iliyoletwa hapà na jina la Lema!
Kwa hiyo kwa kuwa wewe sio Lema hutataka kukosoa unapoona kuna tatizo?
Adui mkubwa wa maendeleo ni fikra potofu na uongozi mbovu, sio majina, dini, kabila au itikadi za vyama!
Rejea tena kumsoma Lema na kama unalo la kupinga hoja yake elezea Ila sio jina!
 
Tanzania Ni nchi rahis Sana kuongoza kama hujui, wale wale waliokuwa wanamsifia mkwere ndio hao hao wanaomsifia Magu, wala hakuna anaehoji intentions zao,anyways...Kidogo Magu anaharibu kujenga system yake, Sasa hata hajamaliza watu wanaona ashaanza kazi......

Tatizo lipo Kwa jamii yetu....ishazoea wizi, ubadhirifu, na dhiki za kutupwa, kuona kiongozi hata anaongelea tu ni sofa tosha........
Ukwel ni kuwa, Magufuli anajaribu, tumpe moyo na muda ndipo tunaweza m judge....its too early to do that

My humble opinion
 
Kama nataka yule kiongozi akamatwe sasaivi......kwa vyovyote vile watz watakushangilia pasipokuangalia haki imetendeka, hiyo paragraf ya umenena mkuu
nothing new at all.hakuna cha majipu wala chunusi, anachokifanya ni kutoa waliowekwa na utawala wa zamani na kuwaweka anaowata yeye kama raisi mpya!!BTW it's a mindset issue because Anafanya tunayopenda kuyasikia na kuyaona ila siyo tunayotakiwa kuyasikia na kuyaona
 
"Mtu akitimiza wajibu wake haina haja ya kumpongeza" yaani sentensi ya kwanza tu inatosha kuonyesha upeo wako. Kwako hauoni kwamba tumefika hapa kwa sababu watu wengi hawatimizi wajibu wao. hao mafisadi, wanaosaini mikataba mibovu, wala rushwa n.k hawakutimiza wajibu wao tena kwa makusudi sasa kama kwako kutimiza wajibu huoni kama ni kitu basi poa, endelea kuzungusha mikono
 
Mimi natumia kichwa kufikiri, mtu akitimiza wajibu wake kwangu sio jambo jipya mfano mdogo tu unielewe kuhusu kodi kukusanya kodi ni wajibu sio ombi kama walikuwa hawakusanyi kodi ni uzembe/wizi sio jambo jipya la kumpongeza wakati watu ni walewale mfumo ni ule ule.

Jambo jipya kwenye swala la kodi la kupongeza ni kunionyesha vyanzo vipya vya mapato vya awamu ya tano ndo ntakuelewa, viko wapi? Labda tusubiri pili Rais Kikwete aliwasamehe baadhi ya wezi wa EPA wakarudisha fedha lakini hawakupelekwa mpaka leo.

Huyu amesamehe baadhi ya waliokwepa kodi Bandarini (makontena) akawapa siku saba walipe, wakalipa hatujasikia wamepelekwa mahakamani hawa Magufuli na Kikwete hawana tofauti yeyote katika eneo hili nipongeze nini? Namsubiri atekeleze wajibu wake kama anaweza kwa maoni yangu; Shekhe ni yule yule kanzu imebadilika.

Hivi nina furahia nini iwapo serkali ya CCM kupiitia shirika letu TANESCO walikuwa wanatuibia sh 6000/ na yeye akiwemo kwa ajili ya fomu ya maombi ya awali ya Umeme? Mwacheni Magufuli atimize wajibu wake, sio kumsifia mtu kwasababu hatakuibia tena.Ni miaka mingine mitano ya kupoteza kama tutaendelea kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe, ni vyema wakajua mabadiliko tuliyoyapigia kura ni ya kisera kisheria na kifkra .

Hadi sasa anachohangaika nacho Magufuli ni fikra kama wapizani (kuwaza) tu lakini hajafanikiwa kutenda kama wapinzani na nikilitizama hili Bunge la 11 ilivyopangwa sioni hayo mengine mawili yatapitia mlango upi? Maana kufanikiwa kwake kutategemea sana maamuzi yake katika kujenga (Strongly Institution) na siyo umaarufu wa mtu mmoja mmoja wa kutipua majipu badala ya kupambana na ufisadi tusidanganyane CCM ni Magufuli na Magufuli ni CCM.

Nawasilisha CCM ni ile ile
SASA TUNGEMCHAGUA NANI WAKATI UKAWA WALICHUKUA MGOMBEA TOKA CCM ILEILE? TULIA UPOTEZE BOYA KWANZA NDO UJUE KIN CHA BAHARI
 
Back
Top Bottom