Tukidhamiria kukamata ugoni Dar watabaki wangapi?

Tukidhamiria kukamata ugoni Dar watabaki wangapi?

Mitego mizuri ni ile ambapo kila ukichepuka unapata kitobo usoni.
 
Hebu fikiri kwanza....Mahoteli kila kukicha yanajengwa...Ubungo, sinza, kinondoni karibu kila baada ya mitaa miwili mahoteli na Guests je fikiria mwenyewe...Tuna wageni gani hasa wanaokuja kutoka nje ya mkoa wa kulala hoteli hizo?
Kwani sie tumekuwa Brazil kombe la dunia lipo kwetu wageni kila kona ya nchi wanakuja?

Fahamu kuwa hoteli hizi ni za kulala sisi sisi japo tunamajumba yetu...Mwanaume wa kileo km hachepuki anajambo

Kuchepuka kumekuwa majanga ndugu yangu, tena kama umeshaanza ni ngumu kuacha na mbaya zaidi na haya ma-UKIMWI sijui kama tutapona
 
Kumekuwepo mahotel mengi yanajenjwa kila kukicha walengwa wakiwa wageni, lakini kumekuwa tofauti wenyeji ndio wanakuwa wageni, eti mtu anatoka kinondoni manyanya anakwenda magomeni mapipa.

Mgeni huyu anasingizia stress lakini huku akiwa na mke wa mtu aliyeagwa uwanja wa ndege au ubungo kwenda mikoani na kusindikizwa kwa mbwembwe , kumchumu na kumwombea safari njema.

Ghafula Mama anatafutwa mmewe kapata ajari kibaha katibiwa na kuruhusiwa jioni huku mke akilalamikia simu kuishiwa chaji, asubuhi anamkuta Mme anajiandaa kurejea kwenye vipimo.

Ikiwa kila Nyumba ya wageni inawekewa mite go ndoa zitabaki ngapi kwenye hili jiji la raha na karaha.

Ndoa yetu mimi na Kongosho ni moja ya hizo zitakazodumu!
 
Tutabaki tunaofurahia utamu wa Yesu tu, maana vyoote ni ubatili tu:llama:
 
Back
Top Bottom