Tukatae kwa nguvu kuwapokea wataalam wa IT kutoka Rwanda

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,839
20,285
Ndugu zangu huu mpango tuukatae
It is very shame nchi kubwa hivi inabebwa na kuongozwa eti na.kushauriwa na kanchi kadogo kama kalee
Hivi kweli mtu akupe wataalam wa Computer kwa dunia ya leo mtu akishakuweza kwenye kompyuta ndo umekufaa
Tukatae kwa nguvu huu mpango
Ni kichaa tu ndo anaweza kuukubali

Hebu turejee hii habari kabla ya kuchukua hatua yoyote
Askari wa JWTZ mwenye asili ya Rwanda adaiwa kutoroka Tanzania!
Jeshi limesema litatoa taarifa zaidi kuhusu mwanajeshi huyo anayedaiwa kutoroka na nyaraka muhimu za jeshi!!
Source: Mtanzania Jumapili
======
OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.
Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.
Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.
Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).
Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.
Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.
Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.
Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.
Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.
Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.
Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Nini kinamtia Jeuri Kagame?' ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.
Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.
Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.
"Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake; hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi, " alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.
Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.
Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.
"Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];analysis', mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.
"Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili; njoo ofisini Jumatatu (Kesho)," alisema Meja Komba.
Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.
Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.
-Mtanzania-
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
Ata kama blah blah not to that extent
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
nchi ndogo ni kweli lakini kama ina watu wana akili kuliko wewe lazima ukubali. tuwache ujinga.. wakati ubeljiji ikitawala congo au waingeteza wakitutawala ni kwa sababu sisi wajinga. tuwache ujinga kama hatutaki kunyanyaswa na watu kutoka nchi ndogo. watanzania hadi leo wanaabudi uchawi..unakuta mamia ya watu wamezingira mti eti unaongea..ujinga tu.
 
Tutawakataaje wakati dereva hasikilizi abiria alichukua leseni mwenyewe anajua nani akae wapi kwa wakati gani, acha waje watuchungulie vyema mpaka utumo mwembamba wausome.
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
shame on you [HASHTAG]#chokochanel[/HASHTAG] hivi nchi hii tuna shida na watu wa IT? Hatujawahi kuwa na shida kama hiyo
 
Ndugu zangu huu mpango tuukatae
It is very shame nchi kubwa hivi inabebwa na kuongozwa eti na.kushauriwa na kanchi kadogo kama kalee
Hivi kweli mtu akupe wataalam wa Computer kwa dunia ya leo mtu akishakuweza kwenye kompyuta ndo umekufaa
Tukatae kwa nguvu huu mpango
Ni kichaa tu ndo anaweza kuukubali

Nchi kuwa ndogo isiwe hoja
Israel inaingia more than 10times kwaUSA ila wote tunajua us inavyobenefit toka kwa Hebrews
Come up with a better argument
 
Wacha waje , mana developers wa TZ hawana creativity, hawaoni opportunities, wapo na app za umbea, wordpress, app za accounting package basi. Sijaona complex system ambayo inafaida na tija kwa jamii labda max malipo, nayo ni made in tanzania au from majirani?
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
ACHA KUROPOKA OVYO WEWE MWANAMKE,KAZI GANI YA I.T PROF WATANZANIA AWAWEZI KUIFANYA MPAKA HAO WAJE,SIO BURE UYU BABA YENU ANAKITU NA KAGAME WAKE NA LENGO LAO NI KUBADILI MFUMO WA TANCIS ILI WAPIGE VIZURI SIO EEH NGASTUKA
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.

kinachoongelewa hapo ni application ya IT na sio uvumbuzi, Uvumbuzi ni kitu kingine na matumizi ni kitu kingine..

Wataalamu wa Computer Serikalini hutumika kucontrol mifumo na kudesign system zinazoweza kurun hiyo mifumo na kuisimamia, Unapogusa kitengo cha Computer kwenye taifa lolote basi umegusa mhimili muhimu, swali tunauhakika hao wanyarwanda watakuwa Wazalendo kwetu bila kuuza siri zetu kwa mataifa mengine au kuzivujisha kwa taifa lao?..

Si kweli kama hatuna wataalamu wa Computer wanaoweza kurun mifumo na kuicontrol, pia tumeshindwa kusomesha vijana wetu wa kile kitengo pale Makumbusho au kuajili vijana waliosomea haya Mambo kuwaweka pale na kuwapeleka India na USA kupata training za kutosha???
 
Ndugu zangu huu mpango tuukatae
It is very shame nchi kubwa hivi inabebwa na kuongozwa eti na.kushauriwa na kanchi kadogo kama kalee
Hivi kweli mtu akupe wataalam wa Computer kwa dunia ya leo mtu akishakuweza kwenye kompyuta ndo umekufaa
Tukatae kwa nguvu huu mpango
Ni kichaa tu ndo anaweza kuukubali
Jinsi anavyompenda kagame kuliko watanzania unafikiri atakubali?, not to that extent, watch it
 
Kwanini hamjitumi kutafuta hizo kazi kama mnauwezo!?

Uvivu umejaa watanzania, vitu kama uvumbuzi etc nayo tabu kwa wengi...wengi ni blah blah blah bila chochote cha kuonyesha uwezo sababu hawana.
Tuanze na wewe, umebuni nini ambacho/ ambavyo vimechangia maendeleo ya watanzania? Point ya mleta mada ipo nafikiri kwenye information and national security.
 
shame on you [HASHTAG]#chokochanel[/HASHTAG] hivi nchi hii tuna shida na watu wa IT? Hatujawahi kuwa na shida kama hiyo

Eeeeeh eti Shame.... wewe husie hata na akili ya kazi yoyote, jobless mkubwa..na utaendelea hivyo hivyo

Sibadilishi nilichoandika.
 
Daima, huwa nakubali mipango na mikataba na makubaliano mbalimbali ya serikali na nchi zingine ila hili lina ukakasi na ujinga wa kuwaza!!.

Ila hili, la wataalamu kutoka Rwanda serikali inafanya mzaha na usalama wa nchi yetu . Sisemi serikali, nasema nchi yetu pasi kuangalia nani ni nani maana madhara yake yataigharimu nchi nzima na siyo serikali pekee.

Na ni ujinga tena ujinga wa kiwango cha bombadier!!

Jamaa, mwenye asili ya Rwanda inasemekana hadi leo hatujui alipo na alikuwa kwenye kitengo icho hicho cha ICT na Computer, kwa hiyo tumeona hiyo haikutosha tunawakaribisha kwa mikono miwili ili wajichukulie kama vile wanakula ugali kwa mlenda eeeh!?

Nchi na serikali tukatae huo upuuzi wa kuleta wanyarwanda kufanya ICT hapo Tanzania.

Mfano, wanafunzi tu wanaosoma hapo Tanzania kwenye vyuo vyetu wanafanya "espionage" kila kona walipo bado, tunaona hiyo ni sawa tunataka kuleta wadukuzi eeeeh!?

Tuwakate miguu popote watakapo wekwa.
 
Hili swala likiruhusiwa kuanzia leo nitaamini mkuu ni wa kwao kama watu wanavyo sema sema,kwa kipi ambacho serikari imetaka kutoka kwa wataaramu wa I.T wa hapa ikakosa kama kuna app serikari inataka kutoka huko kwanini tusipeleke wataalamu wetu huko?hii ni aibu kwetu na itatugharimu
 
Back
Top Bottom