Tukatae kuwa mateja wa siasa

Tukatae kuwa mateja wa siasa

greuben

Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
42
Reaction score
4
Kuna wakati mwingine huwa najiuliza nakosa majibu, kwa mtizamo wangu nilidhani watanzania tuwamoja, lakini tuna mfumo wa vyama vingi. Kuwa na vyama vingi hakumaanishi tuchukiane, tutukanane, au tumuone mwingine hafai kwa sababu ya chama chake. Kwani mwisho wa siku sisi tunabaki kuwa wa tz, wanasiasa tuwasikilizeni bila ushabiki na tuwapime kwa hoja na ilani zao bahati nzuri sana wengi tunaelewa wa mambo tunaweza kuwachambua kwa kazi zao.

Jambo moja ambalo nataka kusisitiza hapa, naomba tuache ushabiki na kufanywa kuwa mateja wa siasa, nalisema hili kwa sababu tukichagua kama mateja wa siasa itatugharimu maisha yetu kwa miaka 5, lakini nadhani kwa macho yetu tumeona wengi wako kimasilahi ndio maana tunaona wanasiasa wanagawana vyeo hata kabla hajaingia ikulu, kwa maana kwamba maslahi yao kwanza ya wana nchi badae


mungu ibariki afrika, mungu ibariki Tanzania

asanteni kwa kunisikiliza........sio lazima niitishe press conference
 
Back
Top Bottom