Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Wiki kadhaa zilizopita, ugonjwa wa ebola uliripotiwa nchini humo na taarifa hizo kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Taarifa ya WHO inasema idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huo DRC mpaka sasa imefikia watu wanne huku idadi ya wagonjwa ikiongezeka na kufikia 43.
Tahadhari iliyotangazwa na serikali ni kuanza kuwapima na kuwafuatilia kubaini endapo wana virusi vya ugonjwa wa ebola wageni wote ambao wanaingia nchini kutokea DRC.
Hatua hiyo ilitangazwa juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, na kusema Serikali imechukua hatua hiyo kutokana na ebola kuzuka DRC.
Ummy alisema wageni kutoka nchi hiyo watasajiliwa na kuwafuatilia hadi wanakoishi ili kujiridhisha kama hawana virusi hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy, mfumo huo unafanywa katika vituo vyote vinavyopitishia wageni, vikiwamo viwanja vya ndege, mipakani na bandarini.
Waziri huyo aliwaasa watendaji wa wizara yake walioko katika vituo hivyo wasifanye kazi kwa mazoea, bali wafanye kazi hiyo kwa ufanisi kuhakikisha hakuna mtu anayetoka DRC anapita bila kuchunguzwa.
Tunaamini kuwa serikali imechukua hatua hiyo kwa wakati mwafaka, na inapaswa kueleweka kuwa uamuzi huo hauna lengo la kuwanyanyapaa watu wanaotoka DRC, isipokuwa kwa ajili ya usalama.
Ebola ni ugonjwa hatari ambao unaua watu wengi kwa wakati mmoja, hivyo tahadhari iliyochukuliwa na serikali ni sahihi kwa kuzingatia kuwa DRC inapakana na Tanzania na vilevile kuna mwingiliano mkubwa wa raia wa nchi hizo mbili, hivyo ni rahisi sana kuingia nchini ikiwa hakutakuwapo na tahadhari.
Athari za ugonjwa huo zinathibitishwa na mlipuko wa homa hiyo mwaka 2014 ulivyoua watu zaidi ya 1,000 katika mataifa ya Afrika Magharibi ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Wakati wa janga hilo jumuiya ya kimataifa ililishughulikia kwa pamoja, ikiwamo kupelekwa kwa timu za madaktari kutoa matibabu kwa lengo la kuudhibiti usisambae zaidi na kupelekwa kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu kusaidia.
Hatua nyingine ilikuwa WHO kuyashauri mataifa jirani kuifunga mipaka yao na Guinea, Sierra Leone na Liberia. Kutokana na uamuzi huo ndiyo maana hatua iliyochukuliwa na Tanzania dhidi ya wageni kutoka DRC ni sahihi.
Tunaamini kuwa watumishi wa Wizara ya Afya walioko katika maeneo yote ya vituo vya kuingia nchini wamepokea maelekezo hayo na watafanya uchunguzi na kuwafuatilia raia wote kutoka DRC.
Licha ya kutakiwa kuwafanyia uchunguzi raia hao, lakini dalili za awali za mtu mwenye ugonjwa wa ebola ziko wazi zikiwamo kuwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa misuli, kuumwa na koo, kutapika na kuvuja damu.
Ni matumaini yetu kuwa maagizo aliyoyatoa Waziri Ummy yatatekelezwa haraka ili kuwaepushia Watanzania hatari ya janga la ebola, yakiwamo ya kuandaa timu ya wataalamu, kununua vifaa kinga na vya kutambua wagonjwa na kuimarisha mfumo wa kufuatilia wagonjwa.
Suala lingine la muhimu ni kuwa wageni kutoka DRC watakaofanyiwa uchunguzi na kuonekana wana dalili za ebola wasiruhusiwe kuingia nchini, hivyo warejeshwe kwao.
Tunaona kuwa timu ya wataalamu ihimizwe kuwa na umakini katika kutekeleza jukumu hilo kwenye vituo vyote vilivyoko mikoa ambayo inapakana na DRC.
Chanzo: Nipashe