Makuzi ya binadamu hupitia hatua moja muhimu sana lakini ambayo ni hatari pia 'foolish age' ni katika kipindi ambapo mhusika wazazi au walezi wasipokuwa makini MTU anapotea na kuharibikiwa
Lakini ni katika umri huo pia watu huanza kupata ladha ya mapenzi kuchanganyikiwa na kuzama kabisa kwenye dimbwi la mapenzi lakini mwishowe ujana huisha na watu huachana au hutengana kwa sababu mbali mbali ikiwemo masomo kazi nk
Mapenzi ya ujanani ni hot na ni matamu mno lakini hatimaye tunaoa na kuolewa na watu tofauti kabisa na wapenzi watu wa kwanza/ wa zamani
Mzunguko wa maisha hutukutanisha tena na kuanza kukumbushana mengi, Wengine watu tukiwa kwenye ndoa tayari lakini kwa ujinga wa Wengi bila kuheshimu viapo vyao vya ndoa na nadhiri zao za uaminifu hudanganyana kuwa 'tukakumbushie'
Kuna coincidence mbaya sana katika maisha siku mnapokumbushiana kupasha kiporo ndo siku unafumwa na mwenza wako!!! Maskini uaminifu wako wote unapotea na unavuruga mahusiano yako kwa jambo dogo mno
Ukishaingia kwenye ndoa achana kabisa na upuuzi wote wa zamani akikwambia tukapashe kiporo mwambie kimechacha hakitalika