Tujuze ulipataje scholarship yako?

WAR

Member
Dec 16, 2016
49
36
Jamani tusaidiane hapa katika kufahamishana, ni mbinu zipi ulizotumia hadi ukafanikiwa kupata scholarship ya kusoma masters au PhD yako. Kuna wengine tunaaaply kila mwaka na tunakosa, tafadhali karibu kwa mchango wako
 
Nenda mtandaoni faster tu ili inategemea na courses yako kama ni sanaa utasugua benchi hadi uone
 
Jamani tusaidiane hapa katika kufahamishana, ni mbinu zipi ulizotumia hadi ukafanikiwa kupata scholarship ya kusoma masters au PhD yako. Kuna wengine tunaaaply kila mwaka na tunakosa, tafadhari karibu kwa mchango wako
Wabongo wengi tunashindwa kupata hizo nafasi kwa mambo mengi sana. Hatujawekeza kwenye hizi nafasi kikamilifu.

1. English Language Certificate - hili la lugha halina haja ya kuelezea kwa urefu sanaaaaa, ngeli ni tatizo na hawa jamaa wanataka upeleke vyeti vinavyo hibitisha kuwa unawea english ili umudu communication uwapo chuoni, jitahidi upate cheti cha ithibati ya english pale British Council na kisiwe na zaidi ya miaka 2 unapoomba chuo chako. Hii itakusaidia kupata admission na scholarship kwa urahisi.

2. Personal statement - hapa ndio panapo tuangusha sana wabongo, kila chuo au course wana specific format au tuseme wana vitu wanavyotaka wavione kwenye statement yako, hapa wanaangalia preofessional experience, problem solving skills, your achievements, motives, the relevance of program and your national development plans.
Hapa tunachemka sana, hatuwezi kujieleza kiundani hasa uzoefu ulionao na kwanini unaomba hiyo kozi na je utawezaje kuisaidiaje maendeleo ya nchi yako kwa hiyo elimu unayoitaka?

3. Kozi zinazotolewa scholarship ndizo unazooomba? Si kila kozi unayoomba watakupa scholarship, lazima uhakikishe kuwa kozi unayoomba wamelist kwenye scholarship program. Sasa kama unajiombea tu huangalii vigezo na masharti.

4. Ufaulu wa undergraduate. Hili pia ni jambo lakuzingatia sana. Mara nyingi wanaotoa scholarships wanaweka na vigezo vya watu wanaowataka, sikila mwenye cheti atapewa scholarship, hawa jamaa kumbuka mara nyingi wanatoa scholarships kwa watu masikini, hivyo wanajitahidi kutoa kwa wale waliofanya vizuri kidogo kwenye degree zao za kwanza au za pili. Angalau uwe na upper class second division.

5. Idadi ya schilarship wanazotoa. Hapa unatakiwa anagalau ujue wanatoa kwa watu wangapi? Mara nyingi wanasema watatoa kwa watu wangapi, kama hawajasema sivibaya. Sasa unakuta scholarship wanatoa moja, hapo ujue mchuano ni mkali kupita maelezo, wanaangalia watu waliotoka kwenye vyuo vinavyojulikana sio haya mavyuo yetu na hovyohvyo, au uonyeshe uhodari katika sehemu kama za personal statement sehemu nyingine. Mara nyingi jitahidi kuomba scholarship program ambazo wanatoa kwa watu wengi, ila usiache kujaribu hata kama wanatoa moja.
..............
 
Hivi mkuuu kuhusu point namba nne ya performance ya degree ya kwanza,kuna scholarship moja wameandka at least uwe na above average results Kwa experience yako hii walimaanisha GPA ipi
 
Niliomba university of south Wales nikapigiwa simu nikaongea nao ila shida ikaja experience na mtu wa kunizamini . Cha msingi cheki scholar ship ambazo hutangazwa na usisite kuziomba.
 
Hivi mkuuu kuhusu point namba nne ya performance ya degree ya kwanza,kuna scholarship moja wameandka at least uwe na above average results Kwa experience yako hii walimaanisha GPA ipi
Average ni tofauti kutokana na nchi na nchi, chakuzingatia mkuu ujitahidi usishuke 3.5 kwenye GPA yako
 
Jamani tusaidiane hapa katika kufahamishana, ni mbinu zipi ulizotumia hadi ukafanikiwa kupata scholarship ya kusoma masters au PhD yako. Kuna wengine tunaaaply kila mwaka na tunakosa, tafadhari karibu kwa mchango wako
Mkuu mm nilibahatika kupata ya Narway, hasa za makampuni na mashirika yanayoendesha shughuli zake Tanzania ni rahisi sana kupata.....

Vigezo:
1. Mara nyingi wanaangalia ufaulu GPA above 3.5 (Upper Second) hapa inategemea na zinapopita zinazopita vyuoni wanapendelea above 3.8

2. Course uliyoomba na inayohitajika kwa muda huo kwa sasa za upande wa Energy, Petreleum Sector, Agriculture, Health, Engineering zinatoka sana kwa Tanzania.
Hapa Australia, Norway, China, Sweeden, UK, Finland, Netherland hizi zinatoa sana kwa Watanzania.

3. Baadhi ya zingine hudai working experience.

4. Personal Statement, jinsi unavyojielezea hapa panahitaji umakini

5. Lugha kwa ujumla hasa zile English test kama IELTS au TOEFL kwa nchi zinazohitaji ni lazima uwe na cheti.

Ni baadhi tu nadhani wengine watajazia
 
Wakuu hata mimi nataka kujua mbinu mlizotumia kupata scholarships za kusoma masters nje ya nchi maana miaka miwili sasa ninaomba bila mafanikio
 
Back
Top Bottom