Kwani aliongelea rushwa lini?
Unayo mifano ya kutuonyesha akiongelea rushwa wakati wowote?
Hivi kweli ni lazima kuanzisha mada humu jukwaani?
Sasa hapa unataka tujadili kitu gani kitakachotusaidia kuondokana na balaa hili lililotukumba Tanzania wakati huu!
Ngoja nikupe dokezo la mada ambayo ukiitengeneza vyema wengi wetu tutachangia.
Anzisha mada ya uhakika kabisa inayoeleza jinsi Samia alivyo msaada mkubwa kwa Kenya katika kuidumaza Tanzania isiweze kushika nafasi yake sahihi kiuchumi Afrika Mashariki.
Mimi nadhani Samia Suluhu Hassan atakuwa ni wakala wa Kenya, aliyewekwa hapa maksudi kabisa kuididimiza nchi hii.
Nasubiri mada yako hiyo muhimu ili nami nije nichangie niliyo nayo juu yake. Ninayo mengi sana!