Mwamba Usemao Kweli
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 744
- 186
Ndugu zangu watanzania naomba nitumie jukwaa hili la JF kuzungumza nanyi kama mtanzania mwengine yeyote ninayeguswa na hali tete tuliyonayo kama taifa.
Kwa ufupi bila kumung'unya maneno TANZANIA inaanguka. Kuanguka huku ni kwa sababu kama taifa kuna mahala ambapo tulifanya makosa na hapo tulipofanya makosa ndio pametufikisha hapa tulipo sasa. Sote tunajukumu la kujadili kwa kina na kufahamu ni wapi kama taifa tumejikwaa na kujikwaa huko tumeteleza na sasa tunaelekea kuanguka kama taifa kama hatua madhubuti hazitochukuliwa kulinusuru taifa lisianguke.
Kwa uchache tu angalieni yafuatayo: -
1. Tanzania ilikuwa moja baada ya kuungana kutoka Tanganyika na Zanzibar 1964. Pamoja na kuwepo kwa tofauti na changamoto mbalimbali katika masuala ya kiserikali, kiuchumi na kisiasa lakini nchi ilikuwa ni moja tu. Kwa sasa tuna Tanzania mbili ile ya Bara na ya Zanzibar. Tuliishi upande wowote wa jamhuri ya Tanzania bila bugudha lakini sasa tumeanza kuona kwamba hili halipo tena. Na hata kama lipo ni kuishi kwa hofu na woga. Ni anguko kwa taifa letu.
2. Tanzania ilikuwa hatuzungumzi masuala ya udini. Sasa tunazungumza masuala ya udini katika redio, magazeti, TV, mitaani, mikutanoni, maofisini na mpaka kwenye nyumba za ibada n.k. Hapo awali watanzania tulioowana na kuchumbiana bila ya kujali dini, lakini sasa hili limeanza kujitokeza na sote tunayashuhudia haya. Ni anguko kwa taifa letu.
3. Viongozi na wananchi iwe wa taasisi ama wa dini yeyote ile hawakuwahi kuuwa wala kuteswa kwa mikakati ya watu kukaa na kupanga mauaji ama kutesa. Lakini sasa inaonekana ni masuala ya kawaida kwa viongozi ama baadhi yetu kuuliwa ama kuteswa. Ni anguko kwa taifa letu.
4. Vyombo vya usalama kutumia nguvu kupita kiasi na kuleta madhara kwa watu wasio na hatia ni matukio yanayoshamiri kwa kasi kupitia visingizio vya kuleta amani na kutuliza ghasia. Haya mambo hayakuwepo lakini sasa ni dhahiri hata pale ambapo sheria za nchi zinafuatwa na wahusika kwa maana ya chama cha siasa ama kikundi cha wanajamii kujaribu kuelezea hisia zao kwa viongozi ama kufanya mkusanyiko wa kisiasa, bado yatajengwa mazingira ya kuhatarisha amani ya taifa letu kwa kupitia vyombo vyetu vya usalama. Ni anguko kwa taifa letu.
5. Kutokuwa na uhakika wa ununuzi wa mazao vijijini kwa wakati na kwa bei inayompa mkulima unafuu wa kimaisha na pia kukopwa kwa wakulima mazao yao na kupelekea watu kukata tamaa na kilimo kama sehemu ya ajira kwa mtanzania aisihie kijijini na hatimaye kufikiria kwenda kutafuta maisha mjini pia ni sehemu ya anguko la nchi yetu.
6. Ufaulu wa watoto wetu katika suala zima la elimu na kushuka kwa ubora wa elimu itolewayo kwa mtanzania ni changamoto kubwa katika taifa letu linalopekea kulifanya taifa letu kuendelea kuzalisha ujinga. Si hivyo tu bali pia ongezeko kubwa la watanzania wasiojua kusoma na kuandika ni sehemu ya mmomonyoko wa ujenzi bora wa taifa letu.
7. Kupata uongozi ni lazima kutumia pesa kama huna pesa huwezi kupata uongozi wa taifa letu na hasa kupitia chama tawala. Huu ni ufa mkubwa sana katika taifa letu na hii inapelekea kupata viongozi wasio na uwezo wa kusimamia vema matatizo yetu kama taifa. Ni anguko kwa taifa letu.
8. Uporaji wa rasilimali za taifa letu (madini, misitu, wanyama pori) ni kati ya mambo yanayoongezeka kwa kasi ya ajabu sana. Rasilimali hizi ni hazina ya pekee kama taifa tumepewa na muumba wetu hauthaminiwi sana kwa kuweka mkakati wa kuhakikisha tunakomesha kama taifa. Hili ni sehemu kubwa ya anguko kwa taifa letu.
9. Rushwa katika taasisi za umma na haki kwa watanzania katika vyombo vya mahakama, polisi vimetoweka na tumebaki kulaumiana na kuona kuwa rushwa ni utaratibu wa kawaida katika maisha yetu kwani hakuna wa kusimamia. Ni anguko kwa taifa letu.
10. Ukosefu wa ubunifu katika kuanzisha, kusimamia na kuendeleza miradi mikubwa ya kitaifa ya uzalishaji mali kwa makusudi ya kujenga uwezo wa kuajiri vijana wetu haupo na umepotea na tumebaki kuamini kuwa wageni ndio watakaotuletea maendeleo kwa kuja kuwekeza nchini. Ni anguko kwa taifa letu.
11. Mmomonyoko wa maadili kwa wazee na vijana ikiwemo ubakaji, ulawiti, uvaaji wa nguo zisizo sitiri miili yetu ni anguko kwa taifa letu kimaadili.
Ndugu zangu watanzania, tunashuhudia namna ya viongozi tulikuwa nao sasa jinsi wasivyokuwa na utashi wa kutatua kero na shida za mtanzania. Kwani na wao wamebaki kulalamika na kutuonea huruma kwa shida zilizopo na zinazojitokeza.
Viongozi wetu wa leo hii katika Tanzania wamebakia na kazi zifuatazo: -
1. Kuunda tume za kuchunguza na kutoa taarifa.
2. Kuhuzunishwa na matukio na shida zinazojitokeza.
3. Kuagiza jeshi la polisi kuwasaka waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na wahusika wasipatikane.
4. Kuhudhuria mazishi na kutoa rambirambi.
5. Kusafiri safari za kikazi nje ya nchi.
6. Kuzuia na kukandamiza uwakilishi wa wananchi katika chimbo cha kutunga sheria.
Napata shida kidogo na huwa najiuliza Tanzania iliteleza lini na wapi? Na je nini kifanyike kulinusuru taifa hili ambalo kwa hakika linapoteza mwelekeo wake na sasa limeanza kuaanguka.
TUJITAHIDI TANZANIA ISIANGUKE
Tujadiliane JF.
(Mwandishi wa makala haya ni mwanachama hai wa CCM anayeamini katika kweli, haki na uzalendo zaidi).