Tujitafakari,tujisahihishe

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Raisi,japo anaeweza kuwa na vipaumbele vyake,lakini bado anapaswa kutazama sekta zote kwani kika sekta ina mchango wake katika maendeleo ya nchi na ukuaji wa uchumi.

Sekta hizi ni kama vile biashara, uchumi,elimu,afya,kilimo,n.k.

Ukimtazama huyu tuliena sasa,je, anajal umuhimu wa sekta hizi au yeye sekta muhimu kwake ni sekta ya miundombinu tu?

Je, si kweli anaonekana ku-act kama waziri wa miundombinu na ujenzi?

Maswali ninayojiuliza:

Miundombinu mizuri huku ajira zinakufa itasaidia?

Miundombinu mizuri huku sekta ya kibenki inayumba itasaidia?

Miundombinu mizuri huku kilimo kinadorora itasaidia?

Miundombinu mizuri huko biashara zinakufa itasaidia?

Miundombinu mizuri huku watu wanapoteza ajira na hivyo kuwafanya wasikopesheki,itasaidia?

Miundombinu mizuri kwa vijana wasio na ajira na wasiowezeshwa itasidia?

Miundombinu mizuri huku bei ya pembejeo ikipanda,itasiadia?

Miundombinu mizuri huku purchasing power ya watumishi wa umma ikidhoofika itasidia?

Miundombinu mizuri huku sekta ya kibenki inayotoa mikopo ikiyumba,itasaidia?

Sekta ya uchumi ikidorora,fedha hizi tunazokopa kujengea miundombinu hii tutazilpaje?

Miundombinu mizuri bila afya nzuri ya wananchi itasidia?

Miundombinu mizuri huku sekta binafsi inayochangia pato kubwa la Taifab ikiyumba,italipa?

Matajiri wakifilisiki,malori ya kutumia miundombinu hii kusafirishia bidhaa na mazao ya wakulima yatatoka wapi?

Matajiri wakianza kuishi kama mashetani,nani atapanda Air Tanzania kwenda China kununua bidhaa za biashara?

Tujitafakari,tujisahihishe.
 
Ni wakati wake kufanya na kusema atakavyo. Wakati wetu ukifika 2020 na sisi tutamwambia muda wake umekwisha.
 
mtu anayempinga magufuli anapojenga ndiye huyo huyo akipata nafasi kwenda nchi za wengine haishi kupiga selfie kwenye majengo makubwa na madaraja ; au unafikiri hayo yalishushwa? tumieni akili kufikiri.
 
Back
Top Bottom