KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,900
- 36,223
Habari za jumamosi wapendwa......
Kwa neema za Mungu nina hakika sote tu wazima wa afya tele.....na wale walio kwenye mitihani ya maradhi basi Mungu awajaalie uzima wa afya tele.........
Bila ya shaka sote tumekuwa mashahidi wa maneno ya kejeli dhidi ya wanaume yaliyoshamiri nyakati hizi......kama vile wanaume kama mabinti.....mwanaume suruali na mengine mengi yenye kushush heshima ya mwanaume........
Lakini haya mambo hayajazuka tu.....bali kuna mahali yalipoanzia......
Kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba kuna mahali wanaume tumejikwaa.....kuna mahali wanaume tumekosea.....je tunajua kuwa kuna mahali tumejikwaa....!!??? La hasha kwa muendelezo wa matukio ya matukio na misemo ya kudhalilisha wanaume ni kwamba bado hatujui kuwa kuna mahali tumejikwaa....
Kwanza kabisa heshima ya mwanaume imeshuka kwa sisi wanaume kukwepa majukumu yetu......
Kwa kawaida anapotajwa mwanaume....basi mtu anapata picha ya alama ya ushupavu.....ujasiri....ukakamavu na kiongozi....na mwenye kuwajibika kwa mambo anayopaswa kuwajibika nayo......na hiyo ndio sifa kuu ya mwanaume.....
Lakini sasa hivi kimezuka kizazi cha wanaume wasiopenda kuwajibika na kutimiza majukumu yao.....pamezuka kizazi cha wanaume wanaopenda vitu laini....na wasiopenda kujishughulisha.......ndio hao ambao bila aibu wanakuja mitandaoni kutafuta wanawake waliowazidi umri ili kuwalea......
Ndio hao hao tunaowasikia wamezikimbia familia zao kwa visingizio vya ugumu wa maisha na mambo mengineyo yasiyo na kichwa wala msingi......
Ndio hao hao tunawasikia wakijinadi kwa kuzikataa mimba za mabinti walizowapa.....
Kwa muendelezo wa matukio hayo ni mwanamke gani atajivunia kuwa na mwanaume wa hivyo.......ni mwanamke gani atajivunia kuolewa na mwanamme ambaye ameshindwa hata kujitawala mwenyewe au kujiongoza yeye mwenyewe....!!???
Ndio maana siku hizi wanawake hawaoni tofauti kati yao na wanaume....kwani ndio maana wanadai usawa baina yao na sisi....ambapo kiuhalisia hatuwezi kuwa sawa kama wanaume tutarudi katika mstari..........
Kijana wa kiume anapata muda wa kwenda kwenye mazoezi na kujaza misuli lakini anakosa muda wa kukaa na kufikiria hatima ya maisha yake......
Ujinga huu unaanzia kwa mtu mmoja mpaka unafikia ngazi ya taifa....ambapo tunapata taifa la vijana wa kiume wasiopenda kuwajibika bali wanaopenda kufanyiwa na kulalamika kwa kila jambo.......
Tujisahihishe