Tujikumbushe Mpambanaji Yasser Arafat

Tujikumbushe Mpambanaji Yasser Arafat

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,268
arafat_nica11656439_355545c.jpg

Baba wa Mtoto mmoja (Zahwa Arafat), Mohammed Abdel Raouf Arafat al Qudwa al Husseini ndilo jina lake halisi ingawa utotoni alipewa jina la 'Yasir/Yasser' likimaanisha asiye na makuu/Easy Going, Jina ambalo limeshika kuliko hata Jina lake halisi na KUAKISI maisha yake hadi umauti

Mnamo tarehe 12 Oktoba mwaka 2004, Yasir Arafat, alipelekwa Ufaransa kwa matibabu na kulazwa katika hospitali moja ya kijeshi iliyoko kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Paris. Hata hivyo sio tu hakupata nafuu bali hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya zaidi, na mnamo tarehe 11 Novemba mwaka huohuo akafariki dunia hospitalini hapo (Peres akiri Israel ilihusika na mauaji ya Arafat-http://kiswahili.irib.ir/…/29036-shimon-perez-akiri-israel-…)

1. Alizaliwa mwaka 1929 na kuanza harakati za mapambano dhidi ya utawala wa Israel akiwa katika rika la ujana. Mwaka 1946, Yasser Arafat alielekea nchini Misri kwa ajili ya masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Cairo na miaka mitano baadaye alihitimu masomo katika taaluma ya Usanifu Majengo

2. Bada ya Kuhitimu shahada ya Uhandisi Usanifu kutoka Chuo Kikuu cha Mfalme Fahd, Yasir aligeukia siasa na Kuanzisha chama cha Ukombozi cha Polisario (PLO) kwa lengo la kuikomboa Palsetina kwa njia ya mtutu kupitia uporaji wa silaha

3. Mwaka 1965 alirejea Palestina na kuasisi Harakati ya Fat-h ili kupambana na utawala wa Tel Aviv. Miaka minne baadaye alichukua hatamu za kuongoza PLO hadi alipoaga dunia.

4. Huenda unamjua kwa upande wa vita vita lakini ukumbuke aliwahi kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani mwaka 1994 sanjari na Yitzhak Rabin na Shimon Peres....

Kipi Unakikumbuka kuhusu Yasir?
 
Niliangalia Documentary Aljazeera inaitwa"Who Killed Arafat?".Jamaa wanasema Arafat alilishwa radioactive material, Polonium 210.
Suspect No 1.ni Israel.
 
Back
Top Bottom