Tujikumbushe ma misosi yetu ya miaka ya 80!!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Wakuu leo nimekumbuka miaka ileeee ya 80 hasa ktk swala la misosi.
Enzi hizo nilikua nikiishi na wazazi wangu maeneo ya kanda ya ziwa,tulikua tukimiliki ng'ombe kadhaa,mbuzi,kondoo na kuku,mashamba ya vyakula n.k.
Asubuhi breakfast-Uji dona full maziwa na viazi vitamu/njugu za kuchemsha na mahindi.
Lunch-Dona mixer,mtama na muhogo na sato wa kushiba pilipili kwa wingi,mboga za majani pembeni mchicha pori/mgagani/mchunga.Huku nikishushia kwa nusu lita ya mtindi.
Dinner-Kama kawa dona la mixer na nofu la sangara basi weee!mbaya au nzuri zaidi ulikua unalazimishwa kumaliza msosi uliokatiwa,usipomaliza cha moto utakiona why umekula kwa jirani?
Ubwabwa na soda ni mpaka xmas na new year,tena linapikwa kwanza dona mkishashiba mnasafishia tumbo na kaubwabwa.
Skuli ilikua kama 7kms hv from hm.
 
Mbona hii show bado inaendelea? Umehamia wapi ngosha.
 
Sie ilikua uji buruga(wa punje za ngano),ugali yanga + bamia mixer na nyama,usiku wali maharage si unajua tena watu wa pwani?
 
he he he spika, kwenu mlikuwa 'wasomi'
mnakunywa uji?

Sie tunakula ugali kama breakfast(bu ndemi) au kiporo cha wali au viazi vya kuchemsha.

Afu kuna mboga kama mkarango, chubu na mashishanga.

Afu kule hakuna tembele siku ya kwanza nalishwa tembele nilijuuuuta.
 
Sisi hatujatofautiana sana tulikuwa tunakusanya mbolea ya ng'ombe tunaichoma kisha asubuhi tunaota moto huku tumefukia vizi kwenye moto maarufu kama buulu kiazi kinatoka bomba ukienda kuchunga chakula chako kikubwa ni matogo nk
 
Back
Top Bottom