Jamani tuwe macho na matapeli katika ajira. Mimi nimenusurika. Hebu soma hii:
Siku moja nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Dr Joseph Mwakabonga kutoka WHO, Tanzania. Alijifanya kuwa ananifahamu kabisa na aliniita kwa jina japo mimi simfahamu kabisa na sikumbuki kama nimeshawahi kukutana na mtu mwenye jina hilo. Mtu huto aliniambia kuwa WHO wana mradi ambao wanauanzisha hivi karibuni jijiji Dar na hivyo alinipigia kuniuliza kama nitapenda kufanya kazi katika mradi huo. Akanieleza kuwa nitakuwa ninalipwa dola za Marekani 3000 kwa mwezi, nitapewa gari ya kutembelea (Landcruiser VX), nyumba pamoja na marupurupu mengine. Wakati ananipigia alisema alikuwa mkoani Rukwa na alitegemea kuja Dar kwa ndege siku hiyo jioni na akaniomba tuonane kwa mazungumzo zaidi ambapo atangenikutanisha na boss wake na alisema akifika tu Dar atanitafuta.Mimi sikuamini kuhusu hilo dili lakni nilikubali tukutane ili nimsikilize ana kwa ana ili niweze kubaini kama hilo dili ni la kweli au ni usanii .Hata hivyo siku hiyo hakunitafuta. Kesho yake nilimpigia akaniambia yuko Mkuranga kwenye eneo mojawao la miradi ya WHO na akasema angenipigia baadaye. Lakini cha ajabu mtu huyo hajanitafuta tena tangu siku ile na ni zaidi ya mwezi umeshaisha.Siku hizi hata simu yake haipatikani kabisa.
Kilichonitia wasiwasi, siku ya kwanza wakati tunaongea kwa simu aliniuliza kama nina gari na kama nitakuja nayo. Nilimwambia kuwa gari ninayo lakini kwa sababu tulikubaliana kukutana jioni au usiku nilimwambia sitakuja nayo kwa sababu ya kuogopa usumbufu wa foleni. Ninahisi mtu yule alikuwa mwizi wa magari na alipogundua kuwa sitakuja na gari akaona dili limeharibika!
Je, kuna mdau anamfahamu mtu huyo, au kuna mdau mwingine amewahi kukutana na kisa kama hiki?