Wana MMU....Jumapili ni siku ya familiar.
Tunaweza kujifunza maisha ya upendo kupitia kwa mama huyu ambaye nilimuuzia kiwanja maeneo ya Mbezi chenye thamani ya million 130.
Huyo mama ni advocate, baada ya maelewano na maamuzi ya kuamua kununua kiwanja,kitu cha kwanza kukifiria, aliniambia HATAWEZA KUMWELEZA HUSBAND wake mpk hapo atakapokamalisha ununuzi. Nilimuuliza kwa nn?? Asiweze kumshirikisha mumewe?? Alinijibu, anamwelewa husband wake vzr maana ataanza complain kwa nn anunue kiwanja kwa bei kubwa......Baada ya siku tano, tulikamilisha mauziano na kusign mkataba na kulipana pesa bank.
Kitu cha ajabu ambacho sikukitegemea, mkataba wa mauziano ulikuwa na majina mawili. Hii ina maana yeye huyo mama na husband wake ndiyo wanunuzi wa hicho kiwanja. Ingawa pesa ametoa wife tu. Na baada ya siku tatu husband wake alipelekwa na kuonyeshwa kiwanja na mikataba yake.
Je kwa nini wanawake wengi ndani ya ndoa hawawezi kufanya kama huyo mama?? Je kwa nn wanaume hawapendi kuwashirikisha wake zao mambo yao mengi ya maendeleo.? Tatizo nn??:?