Tujifunze Kenya kuelekea 2015

Tujifunze Kenya kuelekea 2015

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,116
Reaction score
34,960
Educhaguzi.jpg

Maoni ya Katuni


Uchaguzi Mkuu wa nchini Kenya umemalizika ambapo Uhuru Kenyatta, wa muungano wa Jubilei, ameshinda kiti cha urais.
Ushindi wa Kenyatta dhidi ya aliyekuwa mshindani wake wa karibu, Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, aliyewania kupitia muungano wa Cord, umefungua historia mpya kwa taifa hilo.

Ikumbukwe kwamba uchaguzi huo, unafuatia ule wa 2007 uliomalizika na kusababisha kutokea machafuko, kiasi kwamba Wakenya wanne, akiwemo Kenyatta na aliyekuwa mgombea mwenza wake, William Ruto, kushitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Lakini mwaka huu, Wakenya wamerejea katika hali ya amani na kutoa mafunzo kadhaa kwa kwa nchi nyingi barani Afrika.

Miongoni mwa mafunzo hayo ni kujitokeza kwa raia wengi kupiga kura. Kwa namna iwayo yote, ulimwengu umeshuhudia jinsi Wakenya walivyojitokeza kupiga kura katika hali ya utilivu pasipo purukshani zozote.

Walipiga kura sita, kuwachagua Rais, Seneta, Mbunge, Gavana, Mwakilishi wa Wanawake na Diwani. Hawakuchoka, ingawa imetangazwa kuwepo uwezakano miongoni mwao waliziharibu kura kwa kuchanganya namna ya upigaji.

Kama hilo lilitokea ni moja ya changamoto zitakazoshughulikiwa na mamlaka husika nchini humo, lakini ni dhahiri kwamba muitikio wa kujitokeza, kutumia haki ya msingi kumchagua kiongozi wa umma, imejionyesha huko Kenya, na inakuwa funzo hata kwa Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa muda mrefu sasa, Tanzania imekuwa moja ya nchi ambazo raia wake wamekuwa wanashindwa kujitokeza, kwa hisia kwamba ‘kura moja' haiwezi kuathiri kuchaguliwa kwa ‘kiongozi wanayemtaka'.

Ni dhana inayopaswa kuepukwa kwa maana kama ingeendekezwa na Wakenya, ni wazi kwamba wangeweza kujikuta wanarudia uchaguzi wa Rais hivyo kuligharimu taifa hilo.

Pili ni sheria ya uchaguzi inayotoa fursa pana kwa mgombea urais kupata zaidi ya asilimia 50, ili kutangazwa mshindi.
Kiwango hicho ni muhimu kwa vile, pamoja na kujenga mazingira ya kurejewa kwa uchaguzi, hali inayoweza kuligharimu taifa, lakini kinatoa ishara ya kukubalika kwa wanachi walio wengi.

Tatu, Wakenya wamejaribu kuweka bayana na kwa uwazi mtiririko wa matokeo ya urais kupitia mtandao wa kisasa, ingawa baadaye ‘ulitibuliwa' na kurejea katika kuhesabu kura wa kutumia mikono.
Pamoja na hivyo, lakini palikuwa na kituo kilichoonyesha jinsi matokeo yalivyokuwa yanaripotiwa, kutoka jimbo moja hadi jingine.

Hapa nchini, mfumo wa kutoa matokeo ya baada ya Uchaguzi Mkuu umebaki kuwa wa siri inayojulikana kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), hadi pale kiongozi mhusika anapotangaza matokeo ya jumla kwa umma.

Yapo mambo mengi ya kujifunza kutokana na Uchaguzi Mkuu wa Kenya, kwamba kama yamefanikiwa kufanyika Kenya kwa ufanisi mkubwa, hakuna sababu kwa Tanzania tukashindwa.

Kwa kusema hivyo, haina maana mfumo wa uchaguzi Tanzania hauna lililo jema kuliko changamoto ama upungufu uliopo kwa upande wa Kenya, la hasha.

Yapo mambo kwa idadi yake, ambayo Kenya inaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Lakini kwa vile hatua za maendeleo zinahusisha kujifunza zaidi kuliko ‘kubweteka', tunahimiza kwamba mambo mema yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu nchini Kenya, yawe fundisho kwa Tanzania itakapofanya uchaguzi wake 2015.

Tuchukue fursa hii pia kuwapongeza Wakenya kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu. Ni imani yetu kwamba utulivu huo utadumishwa pasipo kuathiriwa na hila zinazohusisha uhasama wa aina yoyote ile.

Sasa ni wakati wa kuijenga Kenya mpya kwa kuzika yote yaliyopita ambayo yalileta mtikisiko kama vile ukabila uliosababisha maafa kama ilivyokuwa uchaguzi Mkuu mwaka 2007. Hakika Wakenya wameonyesha ukomavu kisiasa na ndiyo maana uchaguzi huu umefanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu. Bravo Kenya, bravo Wakenya.


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom