Tujiandae kwa uchumi wa kati halisi

Tujiandae kwa uchumi wa kati halisi

mutanim

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2010
Posts
203
Reaction score
77
Hebu thubutu kufikiria, kwa mfano ule ambao mheshimiwa rais JPM aliutoa wakati anaongea na wabunge; kiwanda kimoja cha ongeza thamani ya ngozi, tutegemee bidhaa hizi (products) ni Viatu, mikanda, mikoba ya kike, wallet za kike na kiume, mabegi n.k. hatua moja mbele, tukiweza kutoa ngozi ya kutosha kukidhi mahitaji ya kiwanda, then tunaweza kuanza kuchukua hatua za kibiashara kama taifa, kutoa ruzuku na kuongeza kodi kwa products za aina hii zinazoingizwa kutoka nje.

Hatua inayofuata ni kuongeza ubora na ku mandate wananchi kwa ujumla kuenzi kwa kununua na kutumia bidhaa hizo za ndani.

Tahadhali ni kwamba wale ambao wanao uzoefu wa soko, wanaweza kuja juu ili kugombelezea soko (protectionism) na kulipiza kisasi (retaliation). Lakini tukijiaminisha na kujiweka tayari tunaweza kusonga mbele.

Pili, uje kwenye soko la uvuvi mkublwa; zingatia kwamba mpaka sasa kitoeo cha samaki tunacho pata ni kile kipatikanacho kwa uvuvi hafifu (non sustainable fishing). Ikifanyika ikawezekana, viwanda vya kusindika samaki vitafanya watanzania wapate kitoeo hicho kwa muda mrefu katika mwaka ( siyo wa msimu).

Ajira;

Fikiria ni kwa namna gani vijana wanaosubiri ajira (available human resources) watakavyozipata bila kugombea.

Sasa fikiria vivyo hivyo kwa viwanda vyote vinavyotarajia kuamshwa (redeemed), naweza kufikiria kwamba itafika mahala tutahitaji kuajiri wageni kwa kazi za kawaida ( non experts) kwani vyuo na soko letu la ajira litakuwa consumed.

Sasa jambo la msingi ni kuunga mkono juhudi za Dr JPM na kutokuwa mashaka au pande zisizoleta tija kwa namna yoyote.

Ukombozi ndiyo huu.
 
Ni rahisi kuwa na mawazo ya aina hiyo.Tumekuwa Taifa la kuota ndoto za Maendeleo kwa Muda mrefu,lakini Hatuwezi kuyafikia maendeleo tunayoyatamani kwa maneno tu.Ulishapata fursa ya kutembelea vijiji vya Tanzania?Ukweli ni kwamba kuna kundi kubwa la Watanzania bado wanahangaika kupata walau mlo mmoja wa siku,kama watu wetu wanautafuta mlo wa siku kwa tochi,ni lini watakuwa na huo uwezo wa kuwa na kipato cha kati?

Leo hii mkulima ametelekezwa na Serikali,analima kwa tabu tena kwa jembe la mkono,anajinunulia pembejeo za kilimo mwenyewe,lakini ukifika msimu wa mavuno,serikali inaweka vizuizi vya barabarani kila uchochoro ili kukusanya kodi toka kwa mkulima masikini aliyetelekezwa katika hatua za maandalizi ya shamba lakini wanakimbilia kumkamua kipindi cha mavuno.

Tanzania si DSM na miji mikubwa pekee,ni eneo lote lililo ndani ya mipaka ya nchi yetu,ukiitazama Tanzania kwa jicho la DSM pekee unaweza kudhani upo uwezekano wa kuibadilisha Tanzania kwa usiku mmoja.Hizo ni ndoto za mchana kweupe.

Badala ya kuendelea kuwekeza kwenye miradi mikubwa kama ya barabara na majumba pamoja na madaraja ya kuvuka bahari,ni wakati sasa kwa Serikali kuwageukia wananchi wa kawaida kwa kuwapatia Ruzuku ya shughuli zao za Maendeleo.Ifike mahali badala ya Serikali kuwakopa wakulima mazao yao kupitia mpango wa "Stakabadhi ghalani" ianze sasa kuziwezesha kaya masikini ziweze kupiga hatua walau kwa kutumia jembe la mkono.

Kipindi cha uchaguzi tulishuhudia Tasaf wakigawa fedha kwa kigezo cha kusaidia kaya masikini,kumbe ilikuwa ni gia ya kuwarubuni wananchi wairudishe CCM madarakani.Kama lengo lilikuwa ni kuziwezesha kiuchumi kaya masikini,mbona zoezi hilo lilienda sambamba na kampeni za uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi hatuoni muendelezo wa zoezi hilo?
 
#Zillahender upo sahihi, lkn usisahau pia kuwa uchumi wa kwanza duniani kuna watu hawana makazi, ombaomba, wanalalamikia ujira mdogo, kuwa uchumi wa kati ama wa kwanza haimaanishi wananchi wote wanakuwa nao. Na nahisi kuna mambo mengi huyajui vzr. Tasaf mpango wa kaya maaikini umeanza zamani sana mbn. Na kama sikosei mwandishi kamaanisha kuanzia awamu hii nchi itapata maendeleo aliyosema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom