Tujadiliane na kujifunza kwa pamoja

19 records studio

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
421
1,085
Habari watu wangu wa jukwaa hili la MMU na JF kwa ujumla.

kuna jambo / stori nimeona inafundisha kwa namna moja ama nyingine na hivyo si mbaya endapo mtachangia kwa mawazo tofauti tofauti.

Katika wikiendi ya Jana na juzi nilibahatika kuonana na mama moja ambaye tulifahamiana siku nyingi kidogo katika shughuli fulani hivi, nikaona sio mbaya tutafute sehemu nzuri ya kukaa na kupata mawazo na stori mbili tatu, na hatimaye akanipa stori moja kuhusu upande wa ndugu zake lakini nikaona ina faida na hasara ndani yake.

Alianza kwa kusimulia na majina ambayo nitaya taja humu si husika bali ni kueleza ili stori iweze kueleweka....


Mike ni mfanya biashara wa kilimo huwa ana uza zaidi mazao yake kulingana na ubora wa mazao yake lakini pia ni mchapa kazi mzuri na mtafutaji pesa kwa bidii, mike ana ishi mkoani morogoro ana familia ya mke na watoto wawili,
Mke wake anaitwa Irene, ni mwanamke mzuri mwenye kila hadhi na kila sifa ya kuitwa mwanamke mrembo au mke bora, anajali na kutimiza kila jukumu ndani ya familia,

Katika ndoa hakukosi migogoro na mikwaruzano, tatizo ya familia hii ni upande wa mume / baba ambaye ni mike,
Mike ni mwanaume ambaye hatumii kilevi chochote wala kuvuta sigara, isipokuwa tatizo lake moja tu ( ngono ) au usaliti ndani ya ndoa yake,

Mike hupenda wanawake mara zote huwabadili mithili ya nguo, kuwahonga hela na baadhi ya mazao yake wala si tatizo kwake. Kumwaga mamilioni na laki mbele ya wanawake wala hakumuumizi kichwa mike...!!

ili hali watu wanalia uchumi umekuwa mgumu yeye kwake uchumi ni mwepesi, mike kufumaniwa na mke wake guest na hata nyumbani kwake haikuwa tatizo ni zaidi ya mara 20 anafumaniwa na mke wake, lakini bado aliendelea kuwa na jeuri ya pesa ya kutembea na wanawake tofauti tofauti,

Lakini wahenga walisema " hakuna marefu yasiyo na ncha "
Irene hatimaye alichoka tabia za mumewe akaamua kufanya mapinduzi, kwanza alikuwa ana muandalia chakula kitamu, kumfanyia kila kitu na hata mumewe aliogopa akidhani atawekewa sumu kwenye chakula,
Mkewe kila siku alikuwa mwenye furaha utafikiri hakuna dalili za kufumaniwa ndani yake, mike akaamua kumuuomba msamaha mkewe lakini mkewe akadai hajatendewa kosa awe na Amani, lakini mike akaona huyu mwanamke atamuua maana yupo kimya haongei lolote kuhusu makosa ya mumewe na hata msamaha anadai mumewe hana kosa,

hali hii ilipekea mike kuitisha kikao cha familia hata hivyo irene alikana malalamiko ya mumewe kuwa hana kosa awe na Amani,

miezi ikakatika wiki zikapita siku zikaenda na hata majira yakayeyuka bado mike aliwaza sana juu ya mkewe kusema hana kosa ili hali alimfumania zaidi ya mara 20 akiwa gesti na nyumbani wakiwa fagharani na wanawake tofauti tofauti na kuwahonga kuwapendezesha kuliko mkewe.

Hatimaye umauti ukamfikia mike kwa msongo wa mawazo na presha juu,
Huu ndio ukawa mwisho wa huyu mike mfanya biashara wa mazao, pumzi yake ilifika mwisho mwili wake ukatengamaa na roho.


Majadiliano na maswali.
1. Kwanini wanaume hawaridhiki hata umpe kitu gani..??

2. migogoro na usaliti katika ndoa itaisha lini....??

3. Hela na mafanikio ni chanzo cha ndoa na mahusiano kuvunjika....??

4. Kwanini wanaume hawapendi kuthamini na kuwapenda wake na wapenzi hao.


Ahsanteni sana.
 
majibu;
1- ni uasilia wa mwanaume....usijiumize kichwa
2- migogoro ni changamoto....ukisha RIP....imekwisha
3- sio hela wala mafanikio - ni mmoja kujiona anatakiwa kuwa juu ya mwenzake (hii bidhaa yangu)
4- tunawapenda na kuwathamini sana wake/wapenzi/mademu wetu......ila hamtaki kukubaliana na uasili wetu -rejea swali la kwanza na jibu la kwanza........

furaha yako maisha yako....
 
1.Sio wanaume tu,hata sie wanawake ni vinyonga yaani tunabadilikabadilika mno ndo tulivyoumbwa hivo hakuna aliye mkamilifu.
2.Itaisha tu pale patakapokua na HOFU YA MUNGU kati ya wanandoa..
3.Hela itategemea maana kama mapenzi mwanzo yalijengwa na mhimili wa pesa..yatatakiwa kuwa hivyo hivyo hadi mwisho, kinyume na hapo patachimbika
4.Umegeneralize mno sio wote inategemea na ulikumba lijianaume la jinsi gani, wengi wa wanawake ving'ang'anizi unakuta hupendwi ila tu unajibebesha mimba ili uolewe, jua uko mbeleni utalia kama umetiwa vitunguu machoni. Cha msingi tu ni kuomba Mungu akupe ubavu wako utapendwa na kuthaminiwa hadi basi.
[HASHTAG]#mtazamo wangu[/HASHTAG]
 
1.Sio wanaume tu,hata sie wanawake ni vinyonga yaani tunabadilikabadilika mno ndo tulivyoumbwa hivo hakuna aliye mkamilifu.
2.Itaisha tu pale patakapokua na HOFU YA MUNGU kati ya wanandoa..
3.Hela itategemea maana kama mapenzi mwanzo yalijengwa na mhimili wa pesa..yatatakiwa kuwa hivyo hivyo hadi mwisho, kinyume na hapo patachimbika
4.Umegeneralize mno sio wote inategemea na ulikumba lijianaume la jinsi gani, wengi wa wanawake ving'ang'anizi unakuta hupendwi ila tu unajibebesha mimba ili uolewe, jua uko mbeleni utalia kama umetiwa vitunguu machoni. Cha msingi tu ni kuomba Mungu akupe ubavu wako utapendwa na kuthaminiwa hadi basi.
[HASHTAG]#mtazamo wangu[/HASHTAG]
siku hizi unakuta mmama mtumzima kabisa na mipete kidoleni.ukimtongoza anasema haya..Yupo mmoja ni kama mama yangu sema nyege hazina adabu;nilipewa tunda saaaafi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni nyie ndio tamaa zenu zinatuwakia sisi wanaume.
Hata maandiko yamesema, tamaa ya mwanamke ni kali kwa mwanamume.
Mkiacha kututamani ndoa zitadumu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom