Tujadili kwa pamoja

Tujadili kwa pamoja

zema21

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
619
Reaction score
257
Ajira ni tatizo kubwa linaloikabili dunia na nchi yetu pia!! Viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge na viongozi wengineo kadhaa walisikika wakikiri ya kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu ambalo litalipuka muda wowote! ingawaje hakuna mwenye takwimu wahitimu wengi wa vyuo wapo mitaani wakitembea huku na kule kutafuta ajira, tempo na hata wengine wanatafuta pa kufanya internship pasipo mafanikio....

Wapo wanaoshauri kuwa vijana wajiajiri pasipo kuangalia suala la ukosefu wa mitaji kwa vijana hao..(kujiajiri panahitaji kuwa na mtaji wa vitendea kazi ikiwamo pango jengo la ofisi, vitendea kazi na fedha za kujiendesha mpaka pale business itakapo stabilize, marketing ikiwamo matangazo ya bidhaa/products ukiachilia mbali elimu ya ujasiria mali ambayo vijana wengi wanaikosa!!!

Serikali kupitia wizara ya kazi na maendeleo ya vijana inatoa fedha kwa kila halmashauri kwa ajili ya makundi ya vijana ambao wanataka kujiajiri! lakini tatizo ni kuwa ili upate fedha hizo lazima uwe umejiunga kwenye saccoss ambapo unatakiwa uweke 1/3 halafu ndipo upate mkopo kwa ajili ya mtaji! mathalani unataka kukopa milioni tatu lazima uweke kwanza milioni moja(Jambo ambalo ni gumu saana kwa vijana wanaohitimu vyuoni ikizingatiwa wengi wanatoka katika familia za kawaida na za chini)

hebu tujaribu kufikiria kwa pamoja kama wewe ungepewa nafasi ya kuwa Mkuu wa nchi ungekuja na sera/mipango gani ambayo ingewawezesha vijana wetu waondokane na tatizo hili.. Na waweze kujiajiri/kuajiriwa!!!!
 
Serikali legelege mkuu, poleni sana vijana 2015 ndio jibu lenu! imagne ujeruman mpaka sasa wana idara ya job creation, watu wanawaza waongeze na kukuza vipi ajira kwa vijana wao...
 
Good idea kumbe hata mataifa yaliyoendelea waliweza kuunda kitu kinachoitwa Job creation!!!!!!!!?
Sasa na sisi watanzania tufanye nini?
 
Walete zile hela walizozificha ulaya ili tujenge viwanda tuajiri vijana wetu. Na pia tufungue mashamba makubwa tuajiri vijana wetu. Kweli serekali hii nilegelege, mpaka mihela yote hiyo imeenda kutumiwa na wazungu huko ulaya mlikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom