Kwangu mimi, kadiri wanavyozidi kubanwa na CHADEMA na kukutaliwa na wananchi kunapojidhirisha wazi, ndivyo wanavyozidi kupanic na kutoa matusi...wamekabiliwa na msongo wa mawazo kwa kipindi kirefu pasipo kutafuta tiba muafaka ,sasa wanaugua ugonjwa wa akili.Matokeo yake sasa hawazisumbui tena akili zao kufikiri ..wala hawajali mbinu wazotumia kusaka kura..Nani ,kama yupo,awaeleze watu hawa wajirekebishe, ikiwa kila mmoja ndani ya CCM ni mtaalamu wa mikakati ya siasa .Hata wale ambao hawakupaswa kuongoza eneo lolote isipokuwa familia zao, sasa ndio wanaounda kamati ya ufundi ya kampeni za chama.
Kwa muda sasa,maandishi yamekuwa dhahiri ukutani, lakini kwa kuzoea mvinyo wa utawala,wamemeviza uwezo wao wa kuelewa kilichoandikwa.
Kwa kuwa,kimaadili wananchi hawapendi kusikia matusi,Wana Arumeru, kwa niaba ya watanzania, wamejitolea kuonyesha kwa vitendo chuki yao dhidi ya ukosefu wa staha, utu na heshima ulioonyeshwa na watu wanaopenda kuvalia mavazi nadhifu ya kijani na suruali nyeusi na waliolewa fikra za kutawala milele vichwani mwao.
Toto hili CCM ,kwa kuonyesha utovu mkubwa wa nidhamu, inapendekezwa lipewe suspension kama adhabu.Kwa utukutu wake,linaitwa na wananchi wa Arumeru,likiwa na wazazi ,ndugu,wapambe,wafurukutwa ,jamaa na marafiki zake ,kwenda kuchukua barua ya kusimamishwa masomo ,kwa muda usiojulikana tarehe 1 April.