Tuipe CCM Tena 2015!!!

Tuipe CCM Tena 2015!!!

kitero

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
563
Reaction score
110
Tuwape tena CCM 2015? Ila kabla ya kuwapa tujiulize wamefanya nini kwa miaka 50 tuliyowapa na tumefaidika kwa lipi? Je wenzetu tuliopata uhuru nao au baada ya sisi wako wapi?maana hawachelewi kusema barabara nzuri wamejenga mashule yasiyokuwa na walimu muindo mbinu vyuo vya kata ndege za kukodi ,tunawaza kuongeza safari za mikoani wakati wenzetu wana waza kuongeza safari za nje na idadi ya ndege.

Tuwangalie wenzetu kama Rwanda ,Kenya, Afrika kusini ,Zimbabwe na wengineo.Je Ccm bado wanatufaa ? Tunataka mabadiliko,tunataka elimu, tunataka ajira huduma bora za afya ,viwanda kilimo bora na nchi isiyo kuwa ya mafisadi .Je bado huyu mwali anasifa za kuwa mke bora? Je unaridhika na kiwango chako cha mshahara ulicho pangiwa na serekali yako? Sera za mifuko ya kijamii?

Jf najua kuna vijana wengi huku tuliangalie hili na kuchangia bila kuangalia itikadi za vyama vyetu.
 
Huwezi kuyaona hayo kwa vile macho yako yana utando wa siasa za majungu, vurugu na uongo za baadhi ya wanasiasa wanaopenda kufanya siasa nyembamba.
 
Mwenzako katoa hoja yenye mantiki inayostahili kujadiliwa kwa kina!! Nadhani ni vema ungejadili hoja aliyoitoa. Lakini kwa kauli yako hii, umejidhihirisha wazi kuwa ubongo wako umejaa kimeta cha ufisadi!!
 
Tuwape tena CCM 2015? Ila kabla ya kuwapa tujiulize wamefanya nini kwa miaka 50 tuliyowapa na tumefaidika kwa lipi? Je wenzetu tuliopata uhuru nao au baada ya sisi wako wapi?maana hawachelewi kusema barabara nzuri wamejenga mashule yasiyokuwa na walimu muindo mbinu vyuo vya kata ndege za kukodi ,tunawaza kuongeza safari za mikoani wakati wenzetu wana waza kuongeza safari za nje na idadi ya ndege.

Tuwangalie wenzetu kama Rwanda ,Kenya, Afrika kusini ,Zimbabwe na wengineo.Je Ccm bado wanatufaa ? Tunataka mabadiliko,tunataka elimu, tunataka ajira huduma bora za afya ,viwanda kilimo bora na nchi isiyo kuwa ya mafisadi .Je bado huyu mwali anasifa za kuwa mke bora? Je unaridhika na kiwango chako cha mshahara ulicho pangiwa na serekali yako? Sera za mifuko ya kijamii?

Jf najua kuna vijana wengi huku tuliangalie hili na kuchangia bila kuangalia itikadi za vyama vyetu.
Ni kweli kabla ya kuchangia mada hii ni vema wana JF wakatafakari siyo tu bila kujali itakadi za vyama, bali na pia kutathmini kama mada yenyewe imeletwa na mtu mwenye kutaka kweli mada yake ichangiwe na watu wenye upeo wa kuchambua mambo. Binafsi naona kama mleta mada ana mawazo mgando, mawazo ambayo yamepandwa mbegu za upofu, ukiziwi, fitina, majungu na chuki binafsi. Watanzania siyo wajinga kiasi hiki, cha kutaka kuwalazimisha waseme kile ambacho wewe unafikiria badala ya uhalisia wenyewe. Watanzania wanajua kabla ya uhuru ni watoto wa akina nani walikuwa wakisoma tofauti na hivi sasa, watanzania wanajua kabla ya uhuru ilikuwa ikichukua siku ngapi kusafiri kutoka Dar es salaam hadi mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Mtwara tofauti na leo hii ambapo mtu hutumia masaa matano tu, Watanzania wanajua kabla ya uhuru ni watu gani walikuwa wakifaa nguo za heshima tofauti na sasa hivi, Watanzania wanajua kabla ya uhuru nchi yetu ilikuwa na hospitali na zahanati ngapi na upendeleo wa huduma za tiba ulivyokuwa mkubwa. Ni watu wenye mawazo yaliyolishwa sumu ya kudharau, kubeza kila jambo, kudhoofisha juhudi za maendeleo n.k ndiyo wanweza kuunga mkono hoja yako yenye unafiki wa kutaka kwaseme tofauti n hali halisi.
 
Hawa hawahitaji kupewa hata mwezi,angalia vijana wao wanauza dawa (unga) unaoharibu akili za watato wa masikini, wamepeana ardhi ya watanzania maekari kwa maekARI, Wamepeana viwanda vya watanzania makumi kwa makumi, wamepeana zabuni mamia kwa mamia,wametengenezea ulaji kila kwenye mwaya, waliyoyafanya hayalingani kwa utajiri tulionao, muda wa uhai wa taifa hili na pia ubora wa kilichofanyika haulingani na gharama iliyotumia.........angalia mfano hai barabara zetu, kwa wale wa dsm angalia mbagala, angalia chalinze dsm.:majani7::majani7::majani7:
 
kama tu malalamiko yetu tutayaweka kwenye vitendo badala ya maneno matupu
 
CCM imekufa na kuoza kabisa. Je unataka kuikabidhi nchi kwa chama kilichooza?
 
kiukweli ccm haifai tena kutawala taifa hili manake hakuna lolote lililofanyika zaidi ya unyonyaji uliokidhiri sana na wametengeneza system yao na kama haupo katika system haupati cheo chochote katika serikali yao.
Kama ni barabara za lami hata tusingepata uhuru wakoloni wangetujengea kuliko ccm walivyoendeleza yale ambayo mkoloni wetu alitujengea mfano madaraja makubwa,reli tuliyonayo,baadhi ya barabara za lami zaidi ya kilometer 1800 na sasa ukiangalia kwa miaka 50 tumeongezakama 4000 za lami ambayo haina uimara wowote.
Ccm hajafanya lolote ukilinganisha na miaka 50 ya uhuru pamoja na rasilimali tulizonazo, zaidi ya wao wenyewe kujinufaisha na kuwa matajiri wa ajabu sana .
 
Back
Top Bottom