Tuiangalie Tanzania nje ya vyama vyetu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
21,443
40,537
Tangu baada ya Rais Magufuli kuhutubia Taifa kupitia kwa wazee wa Dar es salaam, nimeona kuna mabadiliko (Twist) kwenye mitizamo ya baadhi yetu humu JF. Tayari ile mitizamo mikali dhidi ya mawazo chanya ya wenzetu imebadilika.

Kuna wale waliokuwa wanaona Magufuli hawezi kukosea, nao wameanza kuona kumbe kwa kuwa Magufuli ni mwanadamu naye pia hukosea. Lakini wapo pia walionza kwa kuamini kwamba Magufuli atafanana kwa kila kitu na Kikwete kiutendaji na kimtazamo, nao pia wameanza kubadili misimamo yao.

Lakini Magufuli ndiye Rais wetu na anaoongoza serikali inayoendeshwa kwa Kodi zetu au inayotokana na dhamana ya nchi yetu. Kama taifa tusipojenga tabia ya kuyatazama matatizo yetu kwa jicho la kitanzania badala yake tukawa tuyachambua na kuyaangalia kwa jicho la misingi ya vyama vyetu hatutapiga hatua Abadan.

Tuangalie kama kweli tunataka kujenga viwanda ni viwanda vya aina gani vijengwe, malighafi yake itapatikana nchi mwetu, itaajiri kiasi gani cha watu wetu, kitaleta aina gani ya teknolojia mpya, kitalipa kodi kiasi gani na kitashiriki vipi kuujenga uchumi wa nchi yetu ili uwe imara?

Kama kuna nyanja mbali mbali tunazotaka ziwe bora kuliko zilivyo hivi sasa tunatakiwa tufanye nini ili ziboreke. Badala ya kurushiana vijembe kutwa kucha, ni wakati wa kutumia mbongo zetu kuibadili Tanzania yetu kwa faida ya sasa na kwa vizazi vijavyo!!

Hata hivyo mpishano wa tafakuri juu ya mambo hayo ni lazima utakuwepo!!
 
hahaha magufuli baba huyu hapa wa kwanza, kesha mtoroka mzee wa kuchunga ng'ombe monduli, haya mleta mada waite na wanywa viroba wenzako wote wa UFIPA, waambie huu si muda wa kulewa bali ni muda wa KAZI TU.
 
Mfumo wa vyama vingi ulikuwepo katika miaka ya sitini lakini ukarudishwa tena nchini mwaka 1992. Tanzania ni zaidi ya itikadi za vyama, ni zaidi ya mawazo ya kisiasa. Hakuna kaburi ambalo linamtambulisha marehemu kama alikuwa ni mfuasi wa chama fulani, nijuavyo mimi kila nafsi ina thamani kuliko hizi harakati za kisiasa. Marekani wanajiita mabingwa wa demokrasia lakini ukiwachunguza kwa undani utagundua kwamba democrat na republican wanaongozwa na mtazamo mmoja katika yale masuala yanayoligusa taifa hilo kubwa.

Sisi tuliotawaliwa na ambao bajeti zetu zinawategemea matajiri wa Ulaya na huko Marekani, eti tunataka kujifanya kana kwamba tunaijua dhana ya vyama vingi kuliko hata hao waliotutawala. Tunatukanana sana hapa Jamii Forum, tunakejeliana bila hata ya kukumbuka kwamba ukipigwa wimbo wa Taifa, wote kwa umoja wetu tutasimama na kuuimba kama watanzania.

Tanzania ni zaidi ya CCM na vyama vyote vya upinzani. Tanzania inaanzia ndani ya roho ya mtu, yale yanayoonekana kwa nje ni matokeo ya ile hali ya mtu kujikubali kwanza. Ndugu zanguni tubadilike, tusijitoe akili kwa sababu ya siasa za bei rahisi, waliotuletea siasa hizi wala hawapendi kugombana kwa sababu ya itikadi zao kutofautiana.
 
hahaha magufuli baba huyu hapa wa kwanza, kesha mtoroka mzee wa kuchunga ng'ombe monduli, haya mleta mada waite na wanywa viroba wenzako wote wa UFIPA, waambie huu si muda wa kulewa bali ni muda wa KAZI TU.
Ndiyo wale wale!
 
Mnaoangalia Tanzania huku mkiwa mnazungusha mikono au kuvaa kofia za njano na t-shirt za kijani ndio mjaribu kubadili fikra na mtizamo wenu.
 
Back
Top Bottom