Tuiache CCM itawale milele: Ufisadi unapogeuka silaha ya kukanyaga demokrasia

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
Nimepaza sauti kwa muda mrefu kuunga mkono mabadiliko - ama uhuru wa pili wa Tanganyika. Lakini baada ya kuchunguza kwa makini propoganda machine ya CCM, nikiri bila kumung'unya maneno kwamba nimeamsha mikono! Tuiache itawale milele kama ambavyo makada wamekuwa wakitamba.

Kwa nini nimeamsha mikono? CCM ndio iliyopanda mbegu ya UFISADI na kuulea, ukastawi na hadi ukakomaa. Mungu awabariki kwa hilo. Wananchi walipozinduka usingizini na kuanza kuwanyooshea vidole, CCM hao hao wakajigeuza na kujinadi kuwa ndio wapiganaji wa mstari wa mbele dhidi ya UFISADI. Na kwa vile wananchi waliishapigika vilivyo na wamejawa na hasira kali, basi CCM wameona huo ni mtaji toshelevu wa kuwarubuni waridhie kupoteza DEMOKRASIA kwa kisingizio cha vita dhidi ya UFISADI!!!!

Matukio yanayoendelea nchini tokea awamu ya tano iingie madarakani yanasikitisha. Tunachekelea lakini tufahamu kuwa tunajichimbia kaburi: Polisi wanapogeuka kuwa kitengo cha CCM badala ya kulinda amani na mali za wananchi, Bunge linapogeuka kuwa idara ya Ikulu badala ya kuwa chombo cha kuhakikisha Ikulu inatimiza wajibu wake kwa wananchi, Mahakama inapoanza kupokea maagizo kutoka Ikulu, Jeshi la Wananchi linapoanza kutishia wananchi.

Taifa linaelekea kusiko na vizazi vijavyo vitatafuta makaburi yetu na kuyatandika mijeledi.
 
Nimepaza sauti kwa muda mrefu kuunga mkono mabadiliko - ama uhuru wa pili wa Tanganyika. Lakini baada ya kuchunguza kwa makini propoganda machine ya CCM, nikiri bila kumung'unya maneno kwamba nimeamsha mikono! Tuiache itawale milele kama ambavyo makada wamekuwa wakitamba. Kwa nini nimeamsha mikono? CCM ndio iliyopanda mbegu ya UFISADI na kuulea, ukastawi na hadi ukakomaa. Mungu awabariki kwa hilo. Wananchi walipozinduka usingizini na kuanza kuwanyooshea vidole, CCM hao hao wakajigeuza na kujinadi kuwa ndio wapiganaji wa mstari wa mbele dhidi ya UFISADI. Na kwa vile wananchi waliishapigika vilivyo na wamejawa na hasira kali, basi CCM wameona huo ni mtaji toshelevu wa kuwarubuni waridhie kupoteza DEMOKRASIA kwa kisingizio cha vita dhidi ya UFISADI!!!!
Matukio yanayoendelea nchini tokea awamu ya tano iingie madarakani yanasikitisha. Tunachekelea lakini tufahamu kuwa tunajichimbia kaburi: Polisi wanapogeuka kuwa kitengo cha CCM badala ya kulinda amani na mali za wananchi, Bunge linapogeuka kuwa idara ya Ikulu badala ya kuwa chombo cha kuhakikisha Ikulu inatimiza wajibu wake kwa wananchi, Mahakama inapoanza kupokea maagizo kutoka Ikulu, Jeshi la Wananchi linapoanza kutishia wananchi. Taifa linaelekea kusiko na vizazi vijavyo vitatafuta makaburi yetu na kuyatandika mijeledi.
Na wewe ni sehemu ya propaganda machine ya CCM?
Baada ya uoza uliouorodhesha ambao umefanywa na unaendela kufanywa na CCM kwa miaka 39 na "maisha bora" ambayo imewapatia wadanganyika wa nchi hii unapata wapi uthubutu wa kusema,"Tuiwache CCM itawale milele"?
Kama wewe si sehemu ya propaganda ya CCM, omba ushauri au matibabu "Mirembe".

Propaganda ya CCM inashinda propaganda ya mkoloni(mjerumani, mwingereza)? Je mkoloni ametutawala milele?

Uliza Nyani Ngabu, nini maana ya upoyoyo?
Ni upoyoyo wa wadanganyika ndio utakaopelekea "vizazi vijavyo vitatafuta makaburi yetu na kuyatandika mijeledi".
 
13490575_1234982613213730_271379292288910971_o.jpg
 
Nimepaza sauti kwa muda mrefu kuunga mkono mabadiliko - ama uhuru wa pili wa Tanganyika. Lakini baada ya kuchunguza kwa makini propoganda machine ya CCM, nikiri bila kumung'unya maneno kwamba nimeamsha mikono! Tuiache itawale milele kama ambavyo makada wamekuwa wakitamba. Kwa nini nimeamsha mikono? CCM ndio iliyopanda mbegu ya UFISADI na kuulea, ukastawi na hadi ukakomaa. Mungu awabariki kwa hilo. Wananchi walipozinduka usingizini na kuanza kuwanyooshea vidole, CCM hao hao wakajigeuza na kujinadi kuwa ndio wapiganaji wa mstari wa mbele dhidi ya UFISADI. Na kwa vile wananchi waliishapigika vilivyo na wamejawa na hasira kali, basi CCM wameona huo ni mtaji toshelevu wa kuwarubuni waridhie kupoteza DEMOKRASIA kwa kisingizio cha vita dhidi ya UFISADI!!!!
Matukio yanayoendelea nchini tokea awamu ya tano iingie madarakani yanasikitisha. Tunachekelea lakini tufahamu kuwa tunajichimbia kaburi: Polisi wanapogeuka kuwa kitengo cha CCM badala ya kulinda amani na mali za wananchi, Bunge linapogeuka kuwa idara ya Ikulu badala ya kuwa chombo cha kuhakikisha Ikulu inatimiza wajibu wake kwa wananchi, Mahakama inapoanza kupokea maagizo kutoka Ikulu, Jeshi la Wananchi linapoanza kutishia wananchi. Taifa linaelekea kusiko na vizazi vijavyo vitatafuta makaburi yetu na kuyatandika mijeledi.

Ya weza kuwa kweli eeeh!? Nimeamka usingizini natafakari!
 
Back
Top Bottom