Tuhuma za ufujaji wa mamilioni ya fedha zawatikisa UVCCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, umeagiza aliyekuwa Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo, Alhaji Omari Kariati, anayetuhumiwa kufuja zaidi ya Sh. milioni 26 za umoja huo akamatwe na kufikishwa mahakamani.

Tamko hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkuu wa umoja huo, uliofanyika katika mji mdogo wa Mirerani baada ya wajumbe hao kutaka kujua hatua iliyochukuliwa dhidi ya katibu hiyo ambaye kwa sasa ni Diwani wa (CCM) Kata ya Kwadelo, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Tuhuma dhidi ya Kariati zimechukua muda mrefu na hivi sasa vijana hao wanadai kuwa Alhaji Kariati amekuwa analindwa na kigogo mmoja wa serikali na hivyo kukwamisha upatikanaji wa fedha zao.​

Akizungumza kwenye kikao hicho, mmoja wa wajumbe, Abdalah Nangu, alihoji ufujaji wa fedha hizo ambazo zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa mradi wa gari la abiria zilizokusanywa Mei 9, mwaka 2010 katika harambee iliyoongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.​

Nangu alisema hawakubali mtu mmoja afuje fedha zao na kwenda kugombea udiwani kijijini kwake bila kuchukuliwa hatua kwa hofu ya kulindwa na kigogo hivyo hivyo alipendekeza Kariati achukuliwe hatua ikiwemo kupelekwa mahakamani.​

Mjumbe mwingine, Ngayaila Samweli, alisema Ahaji Kariati alichukua fedha hizo na kwenda nazo Kondoa kugombea udiwani, lakini anaogopwa kuchukuliwa hatua wakati alichukua fedha zilizochangwa na viongozi wa kitaifa.​

"Hili siyo shamba la bibi, kila mtu aje ajichumie fedha na kuondoka bila kuchukuliwa hatua yoyote. Mtu yupo hapa Kondoa tunashindwa kumchukulia hatua jamani, akamatwe na apelekwe mahakamani," alisema.​

Kwa upande wake, Jacqueline Momo, alitoa wito kwa waziri mmoja (jina tunalihifadhi) kutowashinikiza askari polisi kumlinda Alhaji Kariati pindi alipokamatwa wilayani Kondoa ili akashtakiwe wilayani Simanjiro.​

"Alhaji Kariati alikamatwa wilayani Kondoa ili aletwe huku, lakini Waziri mmoja alipiga simu na kudai kuwa siasa chafu za Simanjiro ndizo zinazosumbua hivyo aachiwe na kisha akaachiwa bila kuchukuliwa hatua yoyote," alidai.​

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, Jamillah Mujungu, aliwataka vijana hao kuendelea kusimama kidete kwenye kudai haki yao na wao wapo nyuma yao katika kuhakikisha kuwa fedha zao zinarudishwa.​

"Hili suala la kusema kuwa wilaya ya Simanjiro kuna siasa chafu siyo jambo jema kwani wakati anachukua fedha za vijana hiyo hali ya hewa ya kisiasa ilikuwa safi, awarudishie fedha zenu," alisema.​

Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Simanjiro, Kiria Laizer, alisema yeye hakunywa hata soda kwenye fedha hizo hivyo asihusishwe kabisa na ufujaji wa fedha hizo uliofanywa na aliyekuwa Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo Alhaji Kariati.​

"Vijana wenzangu tupo pamoja katika kuhakikisha kuwa tunapata fedha zetu na tutamkamata Kariati ili azirudishe kwani nilimkabidhi fedha hizo akazifungulie akaunti benki, lakini hakufanya hivyo," alisema.​

Hata hivyo, Kariati jana alipotafutwa, simu yake ilikuwa imefungwa.​


HABARI NA WOINDE SHIZZA

CHANZO: NIPASHE

4494176400224783024-3135533887853914312









 
Safi sana, magamba yasiyotoka yenyewe lazima tuyang'oe kwa nguvu wakavae gwanda.
 
CCM na Opportunity; Sio Mbaya watu wa CCM kuchota PESA... NI Makosa wengine wakiwa nazo kwa njia ya CCM wanayoitumia?

Ndio Maana wanasema VYAMA VINGINE Havina Uwezo wa kuongoza au KULA VITAMU VYA NCHI KAMA CCM? Tangu liniNa Demokrasia

Yetu... NI LAZIMA UWE NDANI YA NEC YA CCM ILI UPANDE JUU na KUPATA ULAJI; Nani atamwajibisha Mama SALMA kama Mjumbe wa NEC?
 
Siku zote UFISADI ndani ya CCM; masizi ya ulafi na hulka ya udokozi mambo yao yote ni 'Kama Baba, Sawa Mwana'.

Hapo mtu utatuambia nini kuhusu tumaini lolote la chama hiki kuwa bora siku za usoni???????????????? Bure kabisa na wala hamna kitu pale!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tuki wagusa mafisadi papa sio hawa wadogowadogo si lazima nchi itayumba?

Lakini kwa nni na hawa hatukuwapa siku 90?

Safi sana, magamba yasiyotoka yenyewe lazima tuyang'oe kwa nguvu wakavae gwanda.
 
Hawa wanafata nyayo za baba zao mafisadi papa wal sishangai kama jk alivyoshangazwa na umaskini wa watanzania
 
Tuki wagusa mafisadi papa sio hawa wadogowadogo si lazima nchi itayumba?

Lakini kwa nni na hawa hatukuwapa siku 90?

Hao wamepewa zaidi ya 90, leo ni siku ngapi toka watangaziwe kujivua magamba wenyewe?
 
Back
Top Bottom