Tuhuma za Kafulila: Uchunguzi uimeishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za Kafulila: Uchunguzi uimeishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JAYJAY, Aug 5, 2011.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,492
  Likes Received: 823
  Trophy Points: 280
  ni kipindi sasa tangu mheshimiwa Kafulila awatuhumu baadhi ya wabunge kuomba rushwa kwenye kamati ya mheshimiwa Mrema ya serikali za mitaa lakini sijasikia chochote kinachoendelea.

  Hivi wadau, kuna yeyote mwenye taarifa ni nini kinaendelea juu ya hilo suala au ndio wameamua kulinyamazia tu?

  Kwa mtazamo wangu, ni rahisi zaidi hizi tuhuma kuwa na ukweli kwa sababu sioni sababu ya mtu kuwasingia wenzake tuhuma nzito kama hizo bila sababu, labda kama kuna kitu kibaya sana walichomkosea.

  Chama kinaendelea na mchakato wake wa kujivua gamba lakini kama kinashindwa kushughulikia tuhuma kama hizi sielewi mantiki yake iko wapi, je wamewashindwa hawa je, watawaweza wale wenye nyadhifa chamani katika kuwawajibisha, napata mashaka.

  Ila kwa mtaji huu kisitegemee mambo kubadilika kwa sababu kama hawa wendawazimu watakuja kushika nyadhifa kubwa serikalini kama za uwaziri nadhani watatuchinja kabisa kama tu licha ya mishahara mikubwa wanayopata huko bungeni bado wanaendelea na ulafi wao wa kuomba virushwa vidogovidogo huko kwenye halmashauri.
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndugai juzi kwenye mdaharo na lissu alisema uchunguzi unaendelea,subiria.
   
Loading...