Tuhuma 5 bora ambazo hazina majibu

hans2014

Senior Member
Oct 4, 2014
112
99
Wananchi wapo katika "Puzzle" kuhusu tuhuma anazo tumumiwa RC Makonda ambazo mamlaka zifuatazo inabidi zitoe majibu:-

1.Rais-Magufuli aliemteua;
**Alitoa maagizo viongozi wasisafiri nje.
Makonda alifanya safari kwenda Marekani, Ufaransa na afrika kusini.Je zilikua safari za kiserikali?

2.Bunge-wao ndio watunga sheria na wasimazi wa serikali
*na pia alikataa wito wa bunge.

3.Polisi (IGP) yeye ndio ndio mshtaki kupitia ofisi ya DPP, je Makonda alivyoenda kuvamia chombo cha habari IGP alikua na taarifa na akatoa askari na ilikua kwa ajili ya operation gani? Mkurugenzi wa Clouds media katika kipindi cha Clouds 360 alithibitisha kwamba siku ya Jumamosi baada ya siku ya uvamizi (Ijumaa) alisema alienda polisi kutoa taarifa baada ya mitandao ya jamii kudai amekamatwa. Cha ajabu kamanda Sirro mbele ya waandishi wa habari akasema Clouds media hawajiripoti hilo tukio.

4.Tume ya Maadili-RC makonda anatuhumiwa kumikili mali kinyume na taratibu za kiuongozi, Je tume imemchunguza na kupata ukweli?
*Kumiliki magari ya kifahari na nyumba
*Wananchi wapewe taarifa mali anazomiliki RC Makonda

5.TAKUKURU-kupambana na rushwa. Mamlaka ya kuchunguza na kuripoti mienendo ya rushwa kwa kiongozi au raia wa kawaida. Je tuhuma kuhusu RC Makonda mamlaka haioni kuna haja ya kufanya uchunguzi?
*Tuhuma kumuliki magari ya kifahari ambayo mengine alipewa kama zawadi
*Kuwahonga waandishi wa habari ili habari aliotengeneza irushwe katika Tv na kuleta vitisho.

Hizo ni baadhi ya mamlaka zinazotakiwa kutoa majibu kwa wananchi.

Sasa tuangalie tuhuma kumi bora za RC Makonda.

1.Kutoa lugha chafu kwa watumishi wa serikali na kutumia ubabe wakati wa kampeni za "Dar mpya"
2.Tuhuma za kutumia cheti feki au kutumia jina la mtu-ingawa alikua mstari wa mbele kuwafuta kazi wale walifoji vyeti vya shule
3.Kufanya uvamizi kituo cha television kwa kutumia silaha na ushahidi upo
4.Kuanzisha kampeni ya kutaja majina ya wauzaji au watumiahi madawa ya kulevya kinyume cha taratibu hadi pale mteule wake alipomteua mtu makhusi kwa kazi hiyo ambapo hayo yote yameleta taharuki kubwa nchini baada ya watu aliowataja kukutwa hawana hatia

5.Tuhuma za rushwa-kumiliki gari la mtu aliemtaja katika listi ya wauza madawa ya kulevya, kumiliki majumba ya kifahari Dar na Mwanza.

Je, mamlaka hizo zina majibu gani?
 
Tumeshuhudia bado POLISI-IGP wakitumia nguvu kumdhibiti NAPE asiwashukuru wananchi baada ya kuwatumikia kama waziri "SHAME"
 
Tumeshuhudia bado POLISI-IGP wakitumia nguvu kumdhibiti NAPE asiwashukuru wananchi baada ya kuwatumikia kama waziri "SHAME"
Nape anastahili anavofanyiwa coz kusaidia sn kuwafanyia hivo wapinzani....bahati mbaya anegusa pasipogusika kwa mfalme
 
Safari za nje ya nchi za binafsi zimezuiliwa tokea lini?

Uliza upya aisee.
 
Back
Top Bottom