Mwananchi wa chini
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 227
- 599
Binadamu ameumbwa, amefanywa kua na akili, zaidi amepewa uwezo wa kutumia akili hiyo mwenyewe (individuality). Matumizi huru ya akili kwa kila mwanadamu yanapelekea kuwepo na mitazamo tofauti katika kutafakari mambo mbalimbali pia kumefanya kuwepo kwa aina mbalimbali za tabia za mwanadamu. Uwepo wa utofauti katika tafakari za mambo kunapelekea kuwepo kwa migogoro, misuguano, gomvi na aina zingine za ukosefu wa maelewano.
Tumekua tukiingia kwenye migogoro, mabishano na gomvi mbalimbali kwa sababu ya kua na fikra au mitazamo tofauti juu ya mambo mbalimbali. Utofauti huu wa fikra umetufanya tuhukumu matukio mbalimbali kutokana na Sisi tunavyoona na kuyaelewa matukio hayo bila kujali au kumfikiria aliyetenda au aliyesababisha kutokea kwa matukio hayo. Mkanganyiko huu wa mitazamo umekua na madhara mengi katika maisha ya mwanadamu. Pia Kuwepo kwa utafauti wa kifikra kumesababisha watu kukutana na disappointments mara kwa mara. Mfano unaweza ongea kitu fulani mbele ya watu na kutarajia kuungwa mkono ila watu hao wakawa na mtazamo mungine.
Kutokana na hali hii maelewano yatakuwepo kama tutajifunza kuyafikiria mambo katika pande zote kabla hatujahukumu au hatujajibu kwa tulichokiona au kukisikia. Unaposikia kitu au unaposhuhudia kitu basi ni vema kukifikiria kitu hiko kama kilivo pia mfikirie aliyesema au aliyetenda kitu hicho kisha hukumu kulingana na uchambuzi huo ulioufanya..Tumekua Hatutaki kufikiria mambo kama yalivo au kumfikiria ayefanya na kujua kwamba naye pia ana mtazamo kama tulivyo sisi .
-->Tumekua ni watu wa kusikiliza ili tujibu na sio kusikiliza ili tuelewe
-->Tumekua ni watu wa kuhukumu kutokana na imani zetu au mitazamo yetu bila kufikiria imani na Mitazamo ya wengine
-->Tumekua ni watu wa kuhukumu kwa hisia zetu bila kujali hisia za wengine.
-->Tumekua Hatutaki kukubali na kupokea mawazo ya watu wengine
-->tumeshindwa jenga maelewano kisa hatuamini wanachoamini wengine
"Unacho fikilia wewe kinaweza kua sahihi kwako lakini niamini kwa mwingine kikawa sio sahihi"
#Tuheshimiane