DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 302
Mjadala unaoendelea wa kina Zitto na Ben ni wa kukoseana heshima ya chama. Ni mbinu za kutia nuksi kwenye chama hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu 2015. Hakuna chama kinachokosa wasaliti. Lakini mi naamini CDM ina taratibu zake na ikithibitika muhusika anachukuliwa hatua za kinidhamu na ikiwezekana kabisa kufukuzwa chama kama tulivyoona matukio mengi ya baadhi ya viongozi kufukuzwa chama. Lakini kulumbana humu naona ni kuwapa mwanya vyama vingine kujua baadhi ya mambo ambayo wasingestahili kujua kwa sababu za heshima za chama.
Mimi naamini kabisa CDM kuna watu makini sana, kuna watu wenye nia ya dhati ya kuibadilisha Tanzania ya leo. Watu kama hawa wanaolumbana bila ustaarabu badala ya kufikiri namna ya kujenga chama na tena wengine ni viongozi wa juu wa chama ni utomvu wa nidhamu, ni kuaibisha taratibu za chama. CDM haina budi kuwaadhibu.
Tanzania bado ina imani kubwa na chadema. Chadema kuweni na umoja. Jengeni chama.