Tufundisheni uzalendo

Equitable

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2021
Posts
2,124
Reaction score
5,698
Uzalendo ni ule moyo wa kutumikia nchi yako kwa hali yoyote iwe nzuri au mbaya.
Uzalendo hauangalii maslahi binafsi bali maslahi ya nchi nzima.

Kwa hali ilivyo Ukraine nimeona watu wenye uzalendo wakilinda nchi ya tena kwa silaha duni.

Sasa basi nimejifunza kuwa ,unapokuwa kiongozi wa watu inabidi uwafundishe uzalendo kama ifuatavyo.

1. Watendee haki bila kujali rangi dini kabila wala watokako.
2. Waache wachague mtu wanayemtaka. Usiwachagulie.
3. Ajira zitolewe kwa sifa siyo kujuana.
Kwetu hapa likitokea kama la Ukreini

1. Wapo watakaojitolea kwa moyo.
2. Wengi wataona bora viongozi waliopo madarakani watolewe ili wapumue. Hawa ni neutral
3. Wapo watakaosaidia maadui kwa hali yoyote


Naomba lisitukute.
Hakuna kijana atakayeenda kupigana wakati aliomba ajira jeshini akanyimwa
Mungu ibariki Tanganyika
 
Uzalendo unaosema hapa ✔️✔️ lkn sio ule uzalendo wa wazee wa legacy wa awam ya tano!!
 
Uzalendo unaosema hapa [emoji3581][emoji3581] lkn sio ule uzalendo wa wazee wa legacy wa awam ya tano!!
Awamu ndugu ilua kabisa uzalendo. Watu walikuwa wanawaombea mabaya viongozi wao
 
Kwenye nchi yetu watu wengi wanadhani uzalendo ni kuunga mkono harakati, mtazamo na sera za kiongozi mkuu wa nchi. Ukionekana kukosoa unaonekana sio mzalendo.
Binafsi hii inanipa taabu sana. Kwa sababu naamini uzalendo ni pamoja na kusimamia kweli, kuwa huru kutoa mawazo yako kwa mstakabali wa nchi na si kulinda maslahi ya kiongozi aliyekuteua au anayekulipa mshahara; hata kama unaona wazi maamuzi yake hayako sahihi!
 
Yakitokea hapa naona kazi wataachiwa jeshi,huku vijana wote wakikimbilia kwenye mahandaki...Muumba atuepushie mbali.
 
Tanganyika iko wapi? Mbona haionekani kwenye ramani? Halafu uzalendo ni moja ya mbinu alizoleta Nyerere ili atawale kwa amani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…