Tufahamishane Namna ya kuingiza nchini bidhaa za biashara

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Salaam wadau,

Penye miti mingi, hapakosi wajenzi.

Leo naomba kufahamu au kupata elimu toka kwenu wadau, jinsi ya kufanya ninapotaka kuagiza mzigo/bidhaa toka nje ya nchi kwa nia ya kujakufanya biashara hapa nchini.

Nimeona watu wengi wakifanya biashara ya vitu mbalimbali toka China au nchi za ulaya kuingiza nchini Tanzania na kuziuza kama bidhaa.

Vitu kama, Nguo, viatu, vyombo vya majumbani, vipodozi, mashine mbali mbali, TVs, Radio na majiko ya kupikia. Vifaa vya ujenzi, simu za mikononi nk.

Sasa swali langu hapa, sielewi utaratibu wake unakuwaje katika kufanya "clearance". Iwe ni pale Airport au kama utakuja na meli.
Nataka kuanza kwa mzigo mdogo ambao si kontena la hasha, yaani size ya kuanzia kilos 50 mpka 500 hivi.

Niweze tu kufahamu, ni namna gani TRA watanifanyia hesabu na gharama zote za serikali. Usalama wa kupata mzigo wako ukiwa salama. Muda wa kuweza kuutoa mzigo wako.

Je kuna list yoyote ya makato ya kodi inayoonyesha aina fulani za bidhaa, gharama za kodi ni kiasi gani?

Kwa ambao mnauzoefu wa kuingiza bidhaa mbalimbali iwe mpya au used, nisaidieni ujuzi je ni changamoto gani mnapitia Kwnye uagizaji na utoaji wa bidhaa hizi.

Mwisho kabisa, wenye mapenzi mema ili tukue wote kibiashara, je ni bidhaa gani kwa sasa zinalipa vizuri kwa maeneo ya mjini na huko mikoani ambazo zinatoka nje ya nchi.

Ahsanteni sana, nawakilisha ombili hili ni imani yangu nitapata, watu wema wenye uzoefu usio na shaka juu ya jambo hili.

Karibuni sana!!!
 
Mkuu Simu, sijajua gharama za ku clear simu moja ni sh ngapi?
Uzuri wa simu toka July 1 hazikatwi VAT. Hapo kikukwa ni aina gani ya simu unataka ili tukushauri kuhusu masoko yake. Pili kuhusu gharama za usafirishaji nakushauri tafuta Agent wanaosafirisha kwa meli kama kina silent ocean n.k
 
Nimecheki na silent ocean naona km gharama zao ni parefu.... simu moja ni $20, na mzigo mkubwa cubic meter moja ni $400 meli kipimo sio uzito
 
tumia unique cargo ni faster 10 days umepaga simu zako kutoka china bei ni dola 25 zikiwa nying dola 20 namba zao 0768656656
 
Uzuri wa simu toka July 1 hazikatwi VAT. Hapo kikukwa ni aina gani ya simu unataka ili tukushauri kuhusu masoko yake. Pili kuhusu gharama za usafirishaji nakushauri tafuta Agent wanaosafirisha kwa meli kama kina silent ocean n.k
Wabongo hawajapunguza kodi pamoja na kwamba serikali iliondoa kodi
 
Back
Top Bottom