Tufahamishane kuhusu umuhimu wa Papai kiafya

Puna

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
2,526
4,401
Wakuu habari za jumapili!leo naomba tukumbushane kuhusu umuhimu wa papai.
Papai ni tunda la jadi na mmea wa dawa. Hurefuka hadi kufikia meta 7 kwenda juu.

NAMNA YA KUTUMIA
1.Kusafisha majeraha.

Safisha vidonda vichafu kwa maji yaliyondondoshewa utomvu wa papai bichi. Majia yalioyochemshwa yakapoa pamoja na matone ya machache ya papai bichi ambalo liko mtini.

2.Minyoo
Papaine hufanya kazi kwa ujumla,lakini kwa viwango tofauti, kwa kuondoa aina mbali mbali za minyoo ya tumboni,na hata tegu.

Dozi ya utomvu wa papai bichi katika kutibu minyoo
Umri idadi vijiko vya chai
Miezi 6 hadi mwaka 1 1/2
Mwaka 1hadi 3 1
Miaka 4 hadi 6 2
Miaka 7 hadi 13 3
Miaka 14 na kuendelea 4

3.Kama dawa ya kuzuia minyoo na amoeba
Tafuna kipande cha jani la papai (ukubwa:sm 5 x sm 5) kila siku, au tafuna kijiko cha mezani kimoja cha mbegu.

4. Upungufu wa vitamini A,B na C
Kula kwa wingi mapapai yaliyoiva ili kuimalisha vitamin: vitamin A kwa kusaidia macho kuona,vitamin B kwa kuimarisha mishipa ya fahamu, na vitamin C kusaidia mfumo wa kinga dhidi ya maambukizi.

5. Matatizo madogo ya kuhara yanayoletwa na amoeba
(a) Mizizi na majani inajitosheleza yenyewe bila kuongeza chochote. Osha vizuri na katakata kiganja kimoja cha majani ya mpapai.Ongeza lita moja ya maji,chemsha kwa dk 5 na acha yapoe kwa robo saa. Chuja na kunywa kwa siku moja au siku 7.
(b) Tafuna kijiko cha chai cha nbegu za papai mara 3 kwa siku 7.

6.Kuhara damu kwa amoeba
Kijiko cha cha mezani cha mbegu za papai zilizosagwa mara 3 kwa siku 7.

7.Malaria (isiyo kali)
Mimina lita moja ya maji moto kwenye majani mabichi ya papai yatoshayo kinganja kimoja.Chuja baada ya dk 15. Watu wazima wanywe lita 1 kwa siku moja,watoto wadogo,kwa mujibu umri wao kwa siku 7.

magonjwa mengine ni:-
8.Tumbo kuuma kwa kutosaga chakula(indegestion)
9. Kikohozi
10. Matatizo ya ini,homa ya manjano,manjano ya ngozi,na macho yanayosababishwa na nyogo katika damu.
11. Maambukizi kwenye njia ya mkojo.
12. Kusumbuliwa na pumu.
13. Vidonda vyenye vijidudu.
14. Majipu yaliyo wazi, vidonda vyenye vijidudu, au majeraha madogo madogo yanayotoa usaha.
15. Majeraha makubwa yanayotoa usaha.
16. Maambukizi ya mba.
17. Kufanya nyama ngumu kuwa laini.
18. Sabuni mbadala

Lo! nimeshachoka endeleeeni wengine.
 
Namna ya kutumia umevurugavuruga sana mkuu japo lengo ni kusaidia jamii, ahsante lkn
 
hiyo dose ya minyoo haieleweki kabisa, ifafanuliwe vizuri
Mkuu ni kwamba kinachotibu minyoo ni ule utomvu wa papai bichi, iko ivi:-
Gema utomvu(latex) kwa kukata chale kwenye tunda bichi ambalo bado liko mtini alafu tumia kama ifuatavyo:-
Umri wa miezi 6 hadi mwaka 1 ni nusu kijiko kile cha chai.
mwaka 1 hadi 6 kijiko kimoja
miaka 4 hadi 6 vijiko viwili
miaka 7 hadi 13 vijiko vitatu
miaka 14 na kuendelea vijiko vinne
Nb dawa hii hutolewa mara moja,nyakati za asubuhi kabla ya kula chochote.Kumbuka kurudia baada ya wiki kama tahadhari.
HAPO VIPI MKUU UMENISOMA?
 
Cjaona nguvu za kiume hapo
Mkuu hiyo Dawa ya nguvu za kiume chukua karanga mbichi alafu chukua asali mbichi ya nyuki wadogo hakikisha unajiridhisha kuwa hawajachakachua loweka karang kutwa mzima hakikisha karanga zimenyea kabisa, ina nywea asali yote na zile karanga zikabaki kuwa kama kashata.Sasa tafuna taratiibu na kijiko.NB hii dawa kama hauna uhakika na mzingo utaomba poo maana reaction yake si mchezo.
Angalizo achana na michips kuku,sijui soseji siju baga na hayo matakataka ya wazungu ya kwenye makopo.Kula dona au sembe safi na dagaa wako sio mbaya ukiona ugali haupandi mpango mzima kipande cha papa utamaliza kilo mzima kwa kipande cha mia mbili.Kumbuka vitu vya mafuta mafuta sio vizuri na asubuhi piga muhogo wa kuchemsha baada ya wiki heshima inarudi katika ndoa.
Kila kheri mkuu.
 
Mfano maambukizi katika njia ya mkojo, papai kama tiba unatumiaje?
Tafuna kijiko kimoja cha mezani/chai cha mbegu safi za papai lililoiva,mara tatu kwa siku,kwa siku 7-14.
Nb:Hii tiba haitoshelezi kutibu magonjwaa ya ngono.
 
Mfano maambukizi katika njia ya mkojo, papai kama tiba unatumiaje?
Tafuna kijiko kimoja cha mezani/chai mbegu safi za papai lililoiva,mara tatu kwa siku,kwa siku 7-14
NB:Tiba hii haitoshelezi kutibu magonjwa ya Ngono.
 
Wakuu habari za jumapili!leo naomba tukumbushane kuhusu umuhimu wa papai.
Papai ni tunda la jadi na mmea wa dawa. Hurefuka hadi kufikia meta 7 kwenda juu.
NAMNA YA KUTUMIA
1.Kusafisha majeraha.

Safisha vidonda vichafu kwa maji yaliyondondoshewa utomvu wa papai bichi. Majia yalioyochemshwa yakapoa pamoja na matone ya machache ya papai bichi ambalo liko mtini.
2.Minyoo
Papaine hufanya kazi kwa ujumla,lakini kwa viwango tofauti, kwa kuondoa aina mbali mbali za minyoo ya tumboni,na hata tegu.
Dozi ya utomvu wa papai bichi katika kutibu minyoo
Umri idadi vijiko vya chai
Miezi 6 hadi mwaka 1 1/2
Mwaka 1hadi 3 1
Miaka 4 hadi 6 2
Miaka 7 hadi 13 3
Miaka 14 na kuendelea 4
3.Kama dawa ya kuzuia minyoo na amoeba
Tafuna kipande cha jani la papai (ukubwa:sm 5 x sm 5) kila siku, au tafuna kijiko cha mezani kimoja cha mbegu.
4. Upungufu wa vitamini A,B na C
Kula kwa wingi mapapai yaliyoiva ili kuimalisha vitamin: vitamin A kwa kusaidia macho kuona,vitamin B kwa kuimarisha mishipa ya fahamu, na vitamin C kusaidia mfumo wa kinga dhidi ya maambukizi.
5. Matatizo madogo ya kuhara yanayoletwa na amoeba
(a) Mizizi na majani inajitosheleza yenyewe bila kuongeza chochote. Osha vizuri na katakata kiganja kimoja cha majani ya mpapai.Ongeza lita moja ya maji,chemsha kwa dk 5 na acha yapoe kwa robo saa. Chuja na kunywa kwa siku moja au siku 7.
(b) Tafuna kijiko cha chai cha nbegu za papai mara 3 kwa siku 7.
6.Kuhara damu kwa amoeba
Kijiko cha cha mezani cha mbegu za papai zilizosagwa mara 3 kwa siku 7.
7.Malaria (isiyo kali)
Mimina lita moja ya maji moto kwenye majani mabichi ya papai yatoshayo kinganja kimoja.Chuja baada ya dk 15. Watu wazima wanywe lita 1 kwa siku moja,watoto wadogo,kwa mujibu umri wao kwa siku 7.
magonjwa mengine ni:-
8.Tumbo kuuma kwa kutosaga chakula(indegestion)
9. Kikohozi
10. Matatizo ya ini,homa ya manjano,manjano ya ngozi,na macho yanayosababishwa na nyogo katika damu.
11. Maambukizi kwenye njia ya mkojo.
12. Kusumbuliwa na pumu.
13. Vidonda vyenye vijidudu.
14. Majipu yaliyo wazi, vidonda vyenye vijidudu, au majeraha madogo madogo yanayotoa usaha.
15. Majeraha makubwa yanayotoa usaha.
16. Maambukizi ya mba.
17. Kufanya nyama ngumu kuwa laini.
18. Sabuni mbadala

Lo! nimeshachoka endeleeeni wengine.

Mkuu na amini papai ni kibiko, yaani ukiona linavyo lainisha nyama ngumu unaweza kuwa na wasi wasi kwamba linaweza kulegeza tumbo na utumbo mkubwa na mwembamba kumbe walaa! Mungu mkubwa. Shukrani kwa somo.
 
kweli mkuu Papai kiboko asee! Kuna day tulikuwa porin kikaz, Pande za Ludewa, tulinunua nyama ya Ng'ombe, tukaweka papai then tukaiyanika kama dk20, nyama ilikuwa lain sana
 
Inakuwa laini mpaka inatisha, cha ajabu taste ya nyama haibadiriki! Enzyme ya papin (kama sikosei) ina nguvu sana!
 
Mkuu ni kwamba kinachotibu minyoo ni ule utomvu wa papai bichi, iko ivi:-
Gema utomvu(latex) kwa kukata chale kwenye tunda bichi ambalo bado liko mtini alafu tumia kama ifuatavyo:-
Umri wa miezi 6 hadi mwaka 1 ni nusu kijiko kile cha chai.
mwaka 1 hadi 6 kijiko kimoja
miaka 4 hadi 6 vijiko viwili
miaka 7 hadi 13 vijiko vitatu
miaka 14 na kuendelea vijiko vinne
Nb dawa hii hutolewa mara moja,nyakati za asubuhi kabla ya kula chochote.Kumbuka kurudia baada ya wiki kama tahadhari.
HAPO VIPI MKUU UMENISOMA?
ubarikiwe aisee shukrani sana mkubwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom