Tuendelee kuvuna matunda ya CCM dhaifu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Wengine bado wana matumaini na hali ya nchi ilivyo kwa sasa. Wengine tokea mwanzo walipinga na wanaendelea kukosoa mwenendo wa CCM kama chama tawala jinsi kilivyoifikisha nchi katika hali mbaya.

Katika maumbile kuna kuanza, kukua na kusinyaa. Bahati nzuri CCM kama chama kimepitia hatua zote hizo na sasa kinasinyaa rasmi. Na yumkini kama CHAMA TAWALA KWA HATUA YOYOTE ILE ILIYO BASI NCHI NZIMA INAAKISI NAMNA CCM ILIVYO. Najuwa wenyewe wanakasirika na hawataki kusikia maneno haya.

Katika awamu ya tatu na nne ya uongozi wa CCM ilikuwa wasomi na wanasiasa wakikosoa nchi kuoza kwa ubadhirifu wa viongozi na rushwa na CCM kupoteza maadili, wenyewe walikataa na wakijiona watakatifu. Walipinga kwa kila hali na kuwashugfhulikia baadhi ya makada wake kwa kile walichokiita kukidhalilisha chama. Waliacha kufanyia kazi ukweli na kuanza kuwaandama wakosoaji. Nini hatma ya jitihada hizi za CCM ?

Nchi iliendelea kukua katika upotevu na kuacha misingi yake ya asili. Ikafika wakati huwezi kuitenganisha CCM na rushwa na ufisadi. Bunge na Mahkama vilitumika kusafisha watu na kukisaidia chama, na hata pale vyombo hivi vilipoonesha meno basi lazima ilikuwa ni kazi ya VISASI tu na wala si kwa nia njema. Yote haya yanaoonesha uchovu wa CCM.

CCM imeshindwa kutuonesha njia ya wazi tunakotaka kwenda. Inaunga unga ajenda na sera na hazitekelezeki kutokana na udhaifu huu wa asili uliolelewa ndani ya Chama. Misingi ilishavurugwa na sasa tunafaidi udhaifu tu wa CCM.


Kwa mfano ujio wa Rais Magufuli ndani ya CCM ulijaa hila na hiii ilikuwa ni ule ule udhaifu wa CCM wa kulindana na visasi. Iweje kama kuna mtu anaonekana hana sifa na ni fisadi au mla rushwa ashike nyadhifa kubwa kubwa bila kuchukuliwa hatua yoyote? na BAYA ZAIDI WAKATI WATU HAO WANATUMIKA KUISAIDIA CCM WALIPAMBWA na kutetewa kwa kila hali? Hatima yake mchakato wa kumpata mgombea Uraisi ukavurugika na kulindwa kwa maslahi ya watu fulani na leo hii tunavuna udhaifu tu wa CCM.

Leo hii malalamiko kila kona ya nchi si ya bahati mbaya, CCM imetuletea mtu ambaye hakuandaliwa huo ndio ukweli. Na acha tuvune matunda ya CCM dhaifu.

Watabisha wee, lakini wanaona aibu kwa kiongozi wetu kushindwa angalau kuwa na staha ya lugha ya kuongea na hadhira na angalau kuangalia matukio na kutafuta lugha za kupoza watu, hatima yake ahadi za maendeleo hazionekani na angalau kupata lugha za matumaini tu nalo linashindikana kwa nini ?

Majibu ni rahisi tu. Huo ndio uhalisia wa CCM kwamba imechoka na dhaifu. Kwa hivyo acha tuvune matunda ya udhaifu huo.

Tusimuonee Rais Magufuli bure, inawezekana ana nia njema lakini alikosa maandalizi. Katika mahala nchi ilipofika mikononi mwa CCM ni ndoto kuleta mageuzi ya kweli. Kuna misingi haijaguswa na hawataki kabisa kuigusa, Namuonea huruma Rais Magufuli kulibeba gunia la misumari la CCM huku akitamani ligeuke liwe usufi au pamba. Tuilaumu CCM hapa na wala si Rais JPM.

"Udhaifu huzaa dhaifu" mimi nakubaliana na usemi huu. Kila kitu kinalalamikiwa sasa na hakuna mwelekeo chanya kwa siku za karibuni.

Uchumi hauko sawa, biashara hazieleweki, wafanya biashara wanalalamika, wateja wanalalamika, Wafanyakazi wanalalamika, wakulima wanalalamika na makundi mengine yanalalamika.

Alaumiwe nani ? Kwangu mimi huwezi kuiacha CCM na udhaifu wake.



Kishada
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom