LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 29,908
- 47,535
Kumekua na uandishi wa ajabuajabu wa meseji kwenye simu bila kujali unayemuandikia ni nani na ana umri gani. Mfano wa maneno ni xaxa=sasa, p=poa, vip=vipi, na ufipisho usioleta maana halisi ya neno lililokusudiwa. Inaleta shida sana kwa wazee wenye umri mkubwa inabidi aombe msaada wa kusomewa meseji toka kwa aliyemtumia. Huu ni uhuni au ni fasheni ya kuweka herufi mpya? Au ni uvivu wa kuandika neno lililokamilika? Unakuta x imewekwa badala ya s, sasa hapo kapunguza nini ikiwa idadi ya silabi na hirabu ni ilele? Mbaya zaidi mzee anaandikiwa, kwa vijana tunaelewana japo huo uandishi ni wa kihuni.