Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Serikali ya Tanzania imetakiwa kushusha kiwango cha kodi kinachokatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi sambamba na kupandisha kima cha chini cha mshahara kufikia 750,000 ili kuweza kuboresha maisha ya wafanyakazi.
Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA Bwana Nicholous Mgaya amesema wafanyakazi wengi wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kipato kidogo wanachopata huku wakizungukwa na kero nyingi kutoka kwa waajiri wao ikiwemo kulipwa mishahara kidogo.
Mgaya amesema ni vyema serikali katika awamu hii ya tano ihakikishe kuwa sera ya uboreshwaji mishahara inaundwa ili kuweza kuwadhibiti waajiri ambao wanashindwa kufuata sheria na taratibu za ajira.
Mgaya pia amekemea suala la raia wengi wa kigeni kuweza kupewa ajira kwa wingi katika maeneo ya migodi, hoteli zenye hadhi ya kimataifa, viwandani na kwenye shule binafsi na kutaka msako wa kuwaondoa uendelee ili fursa za ajira ziwafikie watanzania.