Tuchungulie hdd kwa undani

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wakuu Nilijipa ka homework ka vitendo ka kufanya

  • kuna vitu gani ndani ya Hard Disk Drive (HDD)
  • HDD ni muunganiko wa tujivifaa gani ?
Katika makororo yangu ya kompyuta nilikuwa nina HDD ya Maxtor ya 20GB amabayo ilikwua mbovu.So nikaamua kuiifanyia upasuaji. Zaidi ya HDD kilichohitajika kingine ni screw driver sahihi.


Yafuatayo ni maelezo ya picha nilizopiga mwenyewe na ufafanuzi wa sehemu mbali mbali za HDD. Kumradhi kwa quality duni ya picha lakini ni matumanini yangu ujumbe uliokusudiwa utaelewekwa bila tatizo.


Kwanza tunaaza kufungua screw zinazoshiikilia kasha


Mara nyingi HDD zina rangi ya shaba. Juu ya HDD kuna maelezo mbali mbali mbali kama ya size, Pembeni kuna Seheumu za HDD kupokea moto kutoka kwneye Power supply. Pia kuna waya (Data bus) ya kupokea data kutoka na wenda kwenye motherboard. HDD zInaweza kuwa ni ya IDE au SATA, SCSI na Fiber HDD.Zaidi ya speed za hizo HDD unaweza kugundua tofauti ati ya ina moja na nyingine kwa kuangali kwenye interface inayotumika. Na tfauti ya interaface inaweza kuonekena kwenye cable zinazotumika.

Srew nyingine zimefichwa kwa ajili ya warranty


Katila kuhakikisha kuwa wanagundua mtu akikiuka masharti ya wararty kuna screw nyingine zinafichwa chini ya label . Kuifungua sccrew hiyo azima uchane label. Ukichana label then warannty hakuna . Hii ni HDD mbovu tunaendelea. Katika picha hii hapo juu kwenye HDD unaweza kuona kuna malezo mengi juu ya HDD husika.Kuna maelezoni jinsi gani HDD inaweza kufanywa kuwa master au Slave, volatage na vitu kama RPM( Rotatiom per minute)



HDD circuit board aka motherbard ya HDD


Circuit board hii ndio kama ubongo wa HDD inayoongoza utendaji kazi wa vifaa mbai mbali viivyomo ndani ya HDD. Nimeipachika(mimi binafsi sio wataalam) jina la motherboard ya HDD .Hapa ukifungua screws zilizoshikilia ubao huu basi unaweza kutenganishwa na kasha la Hard Disk



Mawasiliano ya Circuit board na HDD


Kilichoishangaza hakuna waya waya zinazounganisha HDD na circuit board. Mawasiliano yanafanyika kutumia vitu kama spring.Waliobobea wenye mambo ya electoniki wanaweza kujua sababu ya hili. Alfu huwa najiuliza kwa nn Cicuit bard nyingi zina rangi ya kijani?



Platters and Read/Wrte heads

Ganda/Kasha la juu la HDD likiondolewa tunaona kitu kama kisahani(platter) Hii ndio disk yenyewe. Pia kuna kichwa cha kusoma na kundika data kwenye kisahani. Kwa jina la kitaalam kinaitwa Read/Wite heads. Kisahanikinangara sana na inashauriwa kazi hii ifanyike kwenye chumba kisafi sana. Kama nilivyosema sijali sana sababu hii ngoma ilishaharibika siku nyingi. Kwa lugha nyepesi ufanyaji kazi wa HDD hauna tofauti kubwa sana na ufanyi kazi wa DVD au CD ROM.....



Mkono wa kuandika na Kusoma

Na hapa ndio electroniki za “mkono” unaotmika kuandika na kusoma data kutoka na kwenda kwenye kisahani zilipo. kumbuka utendaji kazi wa haya yote unaogozwa na na circuit board. Nikifikaga hatua kama hii nashindwa kujiita mtaaalam wa ICT. Najiona kama end user tu. Lakini ibongo bongo hakuna noma.... teh teh teh

Na hapo ndipo nilipomaliza postemterm ya marehemu HDD. Kumbe hata postmerterm r ya itu kilichoufa inaweza ukuchukulia uda mwingi.

Kazi hii ilinichukua saa kama moja na mpaka namaliza screw tatu ziipotea kabisa. Unajua tena uswazi. Sijui kama ingekuwa nzima ningeweza kuirudisha barabarani.

Version nyingine ya hii kitu ipo kwenye GYM YA MTAZAMAJI
 
Back
Top Bottom