Tubadili mfumo wa jeshi la Polisi, uliopo umepitwa na wakati

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Hivi ni kweli tumefika hapa kama taifa lililokosa mwelekeo,hatujua tufanye nini. Mauaji kila siku Kibiti mpaka lini,wanaouwawa ni ndugu zetu,inauma sana haijalishi tunahasimiana kiitikadi lakini ni ndugu zetu wanaopaswa kulindwa na kufanya kazi zao bila uoga wala kutishwa.

Nichukue fursa hii kutoa pole kwa mauaji ya kiongozi wa CCM yalitokea huko Kibiti kama ilivyo habarishwa na vyombo vya habari,familia pamoja na chama chake na wana Kibiti wote.

Umuhimu wa polisi jamii sasa unaonekana kama tulivyowahi kulizungumzia huko nyuma,ni ukweli majambazi ni watu tunaoishi nao kwenye majumba yetu ni kweli kupitia polisi jamii vyombo vyetu vya dola vilibaini wahalifu wengi kupitia dhana nzima ya polisi jamii, lakini leo hii kuwaona wananchi kama adui wa jeshi letu ni kufungua wigo mpana kwa wahalifu hawa kufanya watakavyo kwa kutumia udhaifu wa kimahusiano kati ya wananchi na jeshi letu la polisi.

IG Saidi Mwema aliwahi kuizungumzia umuhimu wa polisi jamii kuwa ni suala mtambuka lenye kuweza kujenga mnyororo mrefu wa kimawasiliano katika ya wananchi na jeshi letu. Chain hiyo iliweza kutumika vizuri kuwabaini wahalifu ambao walikuwa wana hatarisha usalama wa wananchi na Mali zao.

Kuifuta polisi jamii kwa matakwa ya kisiasa bila kulichunguza jambo lenyewe kimtazamo hakuleti tija zaidi ya kuzidisha ufa unaosababisha wimbi la uhalifu kuongezeka.

Kuvunjwa kwa polisi jamii kulifuatia na kauli Kali kuwa jeshi hilo halipaswi kuchangamana na raia hali inayoogofya wananchi kushirikiana na jeshi katika kudhibiti uhalifu. Tuliona awamu ya nne ya uongozi wa taifa hili wananchi walivyo kuwa mstari wa mbele kufichua mbinu mbalimbali na kuwafichua wahalifu hao,nchi ilikuwa salama kinyume na hivi sasa.

Tulipaswa kutazama mapungufu ya polisi jamii kwa kuyafanyia kazi kuliko kuufuta mfumo huo wa ulinzi na usalama wa raia na mali zake. Si kila lililoanzishwa na viongozi watangulizi halikuwa na tija, kwa madhara makubwa yanayojitokeza sasa kwa maamuzi mazito kufanywa kwa utashi binafsi na kuupuza mtazamo wengi ndiko kunako ibua hisia za uhitaji wa katiba mpya yenye kujenga vyombo madhubuti vyenye kuisimamia serikali kwa kutokuibembeleza.

Ili tujenge taifa salama na sehemu salama ya kuishi hatuna budi kuufumua mfumo wa jeshi letu litakalo badili mfumo wake kiutendaji kutoka mfumo wa jeshi la kikoloni la kutumia nguvu na kuwa jeshi la kuhudumia wananchi litakalo ibua ulinzi shirikishi.
 
Siasa ndio zinaiharibu polisi. Polisi inatakiwa iachwe ifanye kazi yake kwa uhuru bila kushurutishwa na wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni makada wa ccm. Wakuu wa mikoa wanajifanya wanajua kazi ya polisi kuliko polisi wenyewe matokeo yake wanatumikishwa kwenye matukio yanayofanya wachukiwe mfano ni pale wapinzani waliposema watafanya maandamano ya UKUTA kila mtu alijua polisi walifanya vitisho kwa niaba ya ccm na hata maoni ya wengi mitandaoni yalikuwa hivyo. Polisi iachwe ifanye kazi zake kwa utaalamu sio kwa matakwa ya kisiasa. Wanaoharibu ufanisi wa polisi ni wanasiasa hao hao unaotaka walifanyie madiliko.
 
Mfumo wa jeshi letu hupokea taarifa tu na kuzifanyia kazi iwe kuna weredi au laaa! Saidi Mwema alijitahidi sana kuanzisha ulinzi shirikishi,lakini nguvu kubwa na changamoto alizozifanya kujenga viashiria vya kufikia viwango vya weredi vimezimwa na kauli moja tu ya mwanasiasa,kuwa jeshi haliwezi kuchangamana na raia
 
Tatizo watu hata wawe na akili nyingi kiasi gani wakifika kule wanawaformat ubongo na kuwajaza uji............ga so ndio maana akili zao wote zinafanana
 
Ndiyo maana kuna mambo makubwa hususani ya ulinzi yalipaswa kuwekwa ndani ya katiba na kuwekewa mazingatio ambayo hayatakiukwa kwa utashi wa mtu mmoja. Mtu akiota ndoto tu anabadili utaratibu hata kama hauna tija
 
Back
Top Bottom