Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
Kazi njema na mbarikiwe na kupanda mbegu ya ushindani madhubuti katika nchi yetu. CCM lazima iondoke madarakani!Kila la heri wakuu na mjiandae na uchaguzi wa serikali za mitaa kabisa maana itabidi muanzie hapo ili kuwa na uhakika zaidi 2015
Kutokana na kukubalika kwa Dr.Slaa na sera za chama chetu, Wazee wa Mbezi Juu tukishirikiana na vijana tuna jenga tawi la chama chetu.. Pia tutachukua kadi za uanachama wa wa Chadema. Tunategemea kumwalika Dr.Slaa kuja kulizindua.
Mkuu Mganyizi, nakupa pongezi zangu kwa hii thread yako mkuu. Kama kuna lolote linalowezekana kufanywa na Chadema ni kufungua matawi nchi nzima mijini na vijijini, najua bado kuna mambo mengi ya kufanya lakini kama tutaweza kufanikiwa kwa asilimia kama 60 tu, basi 2015 ccm wakae mkao wa kung'oka hata kwa mbinu chafu.
Tuendelee kufikisha haya maoni yenu kwa viongozi wa juu ili wayafanyie kazi. Mapambano yanaendelea hakuna kulala ndo sifa ya wapiganaji siku zote huwa hawarudi nyuma, ni kupanga plans nyingi za kutosha.
Heko wanambezi, lakini haitoshi Mbezi wala Dar pekee, matawi yafunguliwe nchi nzima, tena haraka iwezekanavyo. Tujiandae kuchukua mitaa na kuishikilia. Aluta continua.