mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Magazeti yetu nayo yaanze kufanya mambo kisomi. Baada yule jamaa Jana kutumia lugha wamekamata kila anayejua na mwenye idea kidogo ya mchakato mzima wa usafirishaji wa hayo madini yanayokwenda kuchenjuliwa ujerumani /Japan /China alishangaa.
Nilitegemea hata waandishi nao waumize kichwa kidogo naona nao wameanguka humohumo.
Inashangaza kutumia lugha ya kukamata kitu ambacho kimelipiwa kodi, kitu ambacho, kilikuwa kiko katika safari halali kabla ya katazo la mkuu wa nchi. Hivi hawa wawekezaji wakiitangazia dunia uhalisia Nani atapenda kuja kuwekeza katika mazingira ya fitna kama haya.
Nilitegemea kusikia serikali imegundua madini zaidi ya hayo walioandikishana ndani ya makontena yaani gold, copper na silver ili wananchi tushirikiane kumsurubu muwekezaji dhalimu badala yake wanaleta vitu vya visivyo na mashiko.
Tuliite koleo koleo na sio kijiko.