Inapaswa na yeye binafsi kukataa sifa na utukufu huo, ili Mungu allye juu akapate kupokea sifa, heshima na utukufu wote.Natambua ya kuwa naye ni muumini wa madhehebu fulani. Kwa hiyo kwa imani yake, ni lazima atambue ya kuwa ni Mungu Muumba wetu, ndiye tu mwenye kustahili hilo, na pia ndiye ambaye mwenye kujua hatima ya kila kiumbe ambacho amekiumba.
Kwake yeye wanadamu wote aliowapa nafasi ya kuishi ni sawa, isipokuwa ni kama mwanadamu hao kwa utashi, akili na pia kwa hiari yao wameamua kufuata kwa dhati, ama unyofu wa maisha na uchaji Mungu, ama kwa hasara yao wenyewe wameamua kuziasi sheria zake za milele.