Tuache kulalamika, Watanzania tuamke

mvujajasho

Member
Oct 27, 2010
33
23
Wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii kulitawaliwa sana na 'malalamiko' toka kwa watanzania juu ya kauli ya makusudi ya mwanamama mkenya katika kongamano la IYLA huko New York Marekani, kuwa pango la Olduvai yalipogundulika mabaki ya binadamu wa kwanza, eti yapo Kenya.
Watanzania wakaendelea 'kulalamika' kuwa sio tu Olduvai, bali wakenya hawa wamekuwa wakiunadi mlima kilimanjaro kuwa uko kwao, kufikia hatua mpaka wa kuuchora na kuweka maandishi ya kuunadi kwenye ndege zao. Kwamba 'eti' wamesema na diamond platinum s ni wa kwao (hahaha), eti hata samatta pia ni mkenya (yeleuwiiii)
Lakini mimi sitaki kuungana na watanzania wenzangu 'kulalamika'. Wakati sisi tunaendelea 'kulalamika' wakenya wanaendelea kufikiria ni nini tena cha bongo kinafaa 'kuwa cha kwao', ili 'tulalamike tena'. Wameshatuzoea, na wataendelea na kautaratibu kao kama kawaida. Hayo 'tunayoyalalamikia' ni madogo, tujiulize haya kuhusu domination ya wakenya kwa wabongo:
1. Kuna wakenya wengi hawalimi, ila wanajua mazao yanayolipa yakisafirishwa kwenda nje na wanajua wapi ndani ya Tanzania yapo. Wanakuja, wanayanunua kwa bei ya pipi, wanayavusha hadi kwao, wanayapaki upya, wanayapiga lebo ya kenya kisha wanaenda kuuza kwa bei ya kufa mtu ulaya na asia.Mwaka jana nilishiriki katika utafiti wa zao la kitunguu kule Mang'ola Arusha karibu machozi yanitoke. Hali ni hiyohiyo kwa mazao mengine. Si kwamba hatujui, si kwamba wakulima wetu hawajui, si kwamba serikali yetu haijui, ila kuna tunachokijua zaidi. KULALAMIKA.
2. Madini ya 'tanzanite' yanapatikana sehemu moja tu duniani. Merirani, Arusha. Ila nobody in the world knows about this place. Kwenye ramani ya mnyororo wa thamani wa madini haya sisi ni mamburura tu, wafalme wa tanzanite ni wakenya. Ila na sisi kwenye 'tanzanite yetu' tunajitahidi KULALAMIKA. Tujipongeze kwa hili (piga makofi na vigelegele tafadhali) Hili limeimbwa miaka na miaka ila aaaaaaa, serikali, wadau wa madini, fofofoooo! Huko wanakopeleka wakenya hayo madini kuna password gani tusiyoijua sisi wakati madini ni yetu?
3. Kwenye utalii ndio vichekesho kabisa. Watalii wanaoingia nchini, asilimia kubwa wanapitia uwanja wa JKIA wa nairobi, kuliko viwanja vyetu nchini. Huko mara wakenya waseme si ruhusa kupeleka magari yetu kuchukua wageni wetu wanaoshukia huko, mara tuwasubirie boda ya namanga, nk. Na haya kila yanapotokea, kama kawa 'tunalalamika' hadi mioyo yetu inapata burudani. Huku nyumbani, hasa hapo kwenye uwanja wa kimataifa ulio karibu kabisa na vivutio vyetu 'Kilimanjaro International Airport' ni vituko vitupu, ada zinazotozwa kwa mashirika ya ndege kutua ziko juu mno, ada inayotozwa juu ya nauli ya msafiri iko juu mno, na hatimaye, mtalii anayekuja kilimanjaro, inambidi ashukie nairobi halafu aje kwa barabara hadi kilimanjaro. Huu ni wendawazimu. Nenda pale KIA kama ushawahi kwenda kwenye viwanja vingine vya kimataifa, utastaajabu, kwa siku nzima zinaweza kutua ndege tatu tu za kimataifa. Tuna wizara ya utalii, tuna bodi ya utalii, tuna wadau wa utalii, na NGO kibao za 'kuendeleza utalii tanzania'. Huko mahotelini tumesharogwa kabisa na wakenya, sehemu kubwa ya management ni wakenya. Na tabia ya mkenya akishafika lazima alete 'dugu' zake wote. Wengi wao ni wajanjawajanja tu. Na tuna vyuo viiiiiiiingi vya utalii vinavyozalisha jobless population. Baadhi ya vyuo hivi vinatoa hadi degree za utalii. Niliwahi kufanya kazi kwenye hoteli moja ya kitalii dar es salaam, meneja wangu mkenya alikuwa na elimu ya certificate ya IT!! Na sina uhakika kama nayo haikuwa ya kuungaunga maana hata kuoperate computer yake ilikuwa ni kila saa Joseee, kuja! Au Sebaaaa kuja! Kazi yake kubwa ilikuwa ni jina la bosi meneja, full stop. Tumeaminishwa kuwa wakenya ni bora zaidi ya watanzania, na kama kawaida, watanzania wanaendelea tu na kautamaduni kao ka unyonge na KULALAMIKA

Imefika wakati sasa tuamke. Tuache kulalamika na tufanye yanayotupasa, ili kizazi kijacho kiyakute haya kama historia. Bila kufanya hivyo tutabakia taifa la KULALAMIKA, daima na milele. Amina
 
Mzee acha kututukana bure. Watanzania wengi tuko makini siku zote. We work and earn our living, and pay government taxes. Unapswa kuwaambia waliokabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi hii (ni wachache sana) ndio failure na wanaopaswa kuamka kwani bado wamelala usingizini. Hayo yote uliyoyasema hapo ni matatizo ya watawala. Leave the honest Tanzanians alone! Au unaogopa kuwa polically correct? usiwahusishe watanzania wote katika mambo ambayo hawana mamlaka nayo.
 
Haya tumeacha kulalamika, hata suala la mameya na uchaguzi wa zanzibar tumeacha kulalamika
 
Bado mnalalamika. Ngoja niwaulize wakuu. Kwa kulalamika kwenu ndio hayo mnayolalamikia yatabadilika au mnaburudisha mioyo? Wewe ni mkulima, unalima na wakulima wenzako kisha mnamuuzia mkenya ambaye anaenda kuuza ulaya, akifanikiwa mnalalamika, kwanini msiungane mkauze huko ulaya wenyewe? Hata hii ni watawala ndio wamelala? Kama jibu ni ndio basi utawasubiri waamke hadi siku unaingia kaburini. Mkuu 'mkwepa kodi' ukilalamika kuhusu ya zanzibar na meya wa jiji ndio hao watawala watamtangaza maalim kuwa rais wa zanzibar au kukubali kirahisi ukawa watwae kiti cha umeya? You dont just complain. Kuna cha zaidi unaweza kufanya, mbaya zaidi inahitajika 'wengi' kuungana na ku-take action. Kwa kulalamika tu, ccm watafanya uchaguzi zanzibar na shein atatawala, na utasahau kama ulilalamika. Kwa kulalamika tu, ccm watawapiga danadana ukawa na mwisho wa siku mkuu wa kaya ataunda tume kuongoza halmashauri ya jiji. Kwa kulalamika tu, wakenya wataendelea kuwa major suppliers wa tanzanite yetu, vitunguu vyetu..... to the global market. AMKA
 
Back
Top Bottom